Mbunge Abood awataka wanahabari kueleza yanayofanywa na rais Samia

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Dokta Abdulaziz Abood amewataka waandishi wa habari mkoani Morogoro Kutumia kalamu zao vizuri kwa kuandika masuala mbalimbali yatakayo leta matokea chanya nchini.

 

Mhe. Mbunge amesema hayo wakati akihojiwa na kituo hiki kuhusu mtazamo wake uhuru wa vyombo vya habari nchini. ambapo amesema wanahabari wananafasi kubwa Kuhamasisha masuala mbalimbali ya kimaendeleo Ili kuunga serikali mkoano katika kuletea maendeleo wananchi.

 

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa kuwaletea maenendeleo wananchi Kwenye sekta ya afya , elimu,barabara na maji lakini baadhi ya watu wanabeza Utendaji kazi wake

Amesema wanahabari Wana kila sababu ya kuhabarisha umma kuwaeleza kila kinachofanyawa na Serikali hasa katika kuwahudumia wananchi Ili watu Wenye nia mbaya na serikali wasipate nafasi ya kusambaza uongo.

 

Amesema Jimbo la Morogoro limepokea fedha nyingi kutoka serikali kuu na kutekeleza miradi ya maendeleo hivyo tuna kila sababu ya kumshuru Dokta Samia hususani ujenzi miradi ya Maji .

Dokta Abood ameongeza Kwa kusema serikali inathamini kazi nzuri inayofanywa na wanahabari katika kutangaza mafanikio ya serikali na kuibua changamoto za Jamii Ili zitatuliww hivyo itaendelea kutoa ushirikiano katika Utendaji Kazi wao.

 

Mhe. Abood ni Mlezi wa chama cha waandishi wa habari mkoa Morogoro (MORO PC) ambapo Leo yamefanyika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari kimkoa ambapo kitaifa yalifanyika Mei 3 jijini Dodoma

 

Katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa chama Cha Waandishi wa Habari mkoa Morogoro Nikson Mkilanya amesema chama hicho kimeadhimisha kwa kupanda Miti mto lukulunge ambao unachangia Maji bwawa la mindu ambapo linategemewa kwa zaidi ya asilimi 70 upatikanaji huduma ya maji Kwa wakazi wa mji wa Morogoro.

 

Amesema mabadiliko tabia nchi yameleta athari kubwa nchini hivyo wanabari wanatakiwa kuunga mkono kwa vitendo mapambano ya uharibifu wa vyanzo vya maji

Related Posts