Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania ni kukuza na kuendeleza amani na usalama barani Afrika ili kukuza na kuendeleza maendeleo ya kiuchumi kwa jamii na bara zima la Afrika. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi wakati akifungua maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika (PSC-AU).
“Napenda kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele kwenye vipaumbele vyetu tulivyojiwekea kama baraza ili kuendelea kutoa ushirikiano kwa nchi zilizojiunga katika baraza”
Maadhimisho yanatoa fursa kwa waafrika kutoa maoni yao ya kuimarisha baraza hilo linaloketi chini ya mwenyekiti wa baraza hilo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.