Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Kapteni
Mstaafu George Mkuchika (Kushoto) sambamba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Wallace Karia (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki
ya NBC, Dk. Elirehema Doriye (wa pili kushoto) wakikabidhi kombe la Ligi Kuu ya
NBC kwa nahodha wa timu ya Yanga SC Bakari Mwamnyeto (Kulia) baada ya timu hiyo
kuwa bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2023/2024. Hafla ya kukabidhi kombe la
ubingwa huo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini
Dar es Salaam wakati wa mechi ya ligi hiyo baina ya mabingwa hao dhidi ya
Tabora United iliyoisha kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3 -0.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC Bw Waziri Barnabas
(kushoto) akikabidhi tuzo kwa mchezaji wa Yanga Aziz Ki aliyetangazwa mchezaji
bora wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara kwa mwezi wa April. Makabidhiano hayo
yalifanyika mapema kabla ya mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Yanga SC dhidi ya
Tabora United uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki ukienda sambamba na hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa wa
ligi hiyo kwa timu ya Yanga. Mechi
hiyo iliiisha kwa
timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3 -0.
Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa Benki ya
NBC Bw Peter Nalitolela akikabidhi tuzo kwa mchezaji wa Yanga Aziz Ki
aliyetangazwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara kwa mwezi wa
April. Makabidhiano hayo yalifanyika mapema kabla ya mchezo wa ligi kuu ya NBC
kati ya Yanga SC dhidi ya Tabora United uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin
Mkapa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ukienda sambamba na hafla ya
kukabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Yanga. Mechi hiyo iliiisha
kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3 -0.
Katika kufanikisha hafla hiyo mwishoni mwa wiki benki
ya NBC mbali na kushirikiana na timu ya Yanga SC kufanikisha baadhi ya matukio
ikiwemo burudani kwenye mkesha maalum wa ubingwa, kuandaa helkopta maalum
iliyoleta kikombe cha ubingwa kwenye uwanja huo, benki hiyo iliandaa hafla
kubwa ya kukabidhi ubingwa huo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa huku ikitoa
huduma mbalimbali za kibenki kwa wahudhuriaji wa tukio hilo ikiwemo usajili wa
uanachama kwa mashabiki wa timu ya Yanga waliofika kwenye uwanja huo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi
wa Hazina na Masoko ya Fedha wa Benki ya NBC Bw Peter Nalitolela (Kulia)
wakijipongeza kwa kufanikisha hafla hiyo.