Marekani na Tanzania Zaungana Kupambana na Usugu Wa Vimelea Vya Magonjwa

Serikaliya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Tanzania leozimeungana kuzindua kampeni yaHolelaHolelaItakukosti ambayo inaratibiwa na Offisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Kampeni hii inazingatia udhibiti kuhusu usugu wavimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA) namagonjwa ya kipaumbele ya zuonotiki (magonjwaambayo yanaweza kuambukizwa kutoka kwawanyama kwenda kwa wanadamu). Kampeni hii yaHolelaHolela Itakukosti inaonyesha umuhimu wakuchukua hatua za kuzuia na kudhibiti usugu wavimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA) namagonjwa ya kipaumbele ya zuonotiki kuanziakatika ngazi za chini kwenye jamii kwa kutoa elimuna hatua za kuzuia maambukizi.

Baadhi ya tabia hatarishi na uelewa mdogo wa kiafyana kisayansi miongoni mwa jamii nchini Tanzaniaunaifanya nchi kuwa katika hatari ya milipuko wamagonjwa ya kuambukiza. Kampeni hii mpyainayohusisha vyombo mbali mbali vya habari itazibamianya ya maarifa na kutoa mifano ya kile ambachojamii inaweza kufanya ili kupunguza kuenea kwamagonjwa au kuugua.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakatiwakuzindua kampeni hii HolelaHolela ItakukostiNaibu Waziri ya Afya, Dkt. Godwin O. Mollelalisema, “Kwa kuongeza uelewa na kuchocheamabadiliko ya tabia, tunaweza kupunguza atharizinazotokana na udhibiti kuhusu usugu wa vimeleavya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA) na magonjwaya kipaumbele ya zuonotiki (magonjwa ambayoyanaweza kuambukizwa kutoka kwa wanyamakwenda kwa wanadamu).

Magonjwa yanayosababishwa na wanyamahuambukizwa kati ya wanyama na wanadamu nahatari kwakua yanaweza kusababisha milipuko namagonjwa ya kuambukiza. Ni muhimu kuzingatia, kutambua, kudhibiti, na hatimaye kuondoamagonjwa haya ili kuhakikisha jamii na wanyamawanabaki wenye afya na kuepuka matatizo yakiuchumi na kijamii. Kampeni yaHolela-HolelaItakukostini mfano mmoja wa jinsi USAID inavyofanya kazi katika jamii kuboresha nakudumisha afya na ustawi wa wote.Alisema Dkt. Mollel.

Kwa upande wake mwakilishi Kaimu Mkurugenziwa USAID Alex Klaits alisema Serikali ya Marekaniinasimama imara katika dhamira yake ya kujengajamii zenye afya bora kwa kuchukua hatua, nakuhimiza kila mmoja kuunga mkono kampeni hii, “Kwa pamoja tusonge mbele kulinda afya na ustawiwa Watanzania wote.”

Related Posts