Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo (kulia), akizunguma wakati wa mahafali ya 18 ya Kitado cha Sita na uzinduzi wa harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa jengo la Tehama lenye thamani ya sh bilioni 1.4 la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Barbro Johansson. Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam Mei 25. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Joha Trust, Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekirti wa Bodi wa shule hiyo, Halima Kamote.
Mwenyekiti wa PTA wa Shule ya Barbro Johansson, Dk. Amini Mshana, (katikati), akizunguma wakati wa mahafali ya 18 ya Kitado cha Sita na uzinduzi wa harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa jengo la Tehama lenye thamani ya sh bilioni 1.4 la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Barbro Johansson. Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam Mei 25. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Joha Trust, Profesa Anna Tibaijuka , Mwenyekirti wa Bodi wa shule hiyo, Halima Kamote na Mkuu wa shule hiyo, Sospina Leonidace(kulia).
Wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson wakitoa burudani wakati wa mahafali yao.