Si Mchezo! Paredi la Yanga lasimamisha shughuli jijini Dar

PAREDI la Kibingwa, linalofanywa na Yanga katika kutembeza Kombe la Ligi Kuu ililokabidhiwa jana, limesababisha baadhi ya shughuli jijini Dar es Salaam kwa muda ili kupisha msafara wa mabingwa hao wanaoshikilia taji kwa miaka mitatu mfululizo sasa na la 30 kwao tangu 1965.

Msafara huo wa Yanga unaoongozwa na Rais wa Klabu, Injinia Hersi akiwa na viongozi wenzake na nyota wa timu hiyo umeanza saa 11:07 asubuhi ambapo wanapita barabara ya Keko kwenda Jangwani yalipo Makao Makuu ya klabu hiyo kongwe iliyoasisiwa mwaka 1935.

Kabla ya msafara huo, wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi, walifika asubuhi na kunywa supu kwa pamoja na mashabiki wao ikiwa sehemu ya kuonyesha umoja wao.

Shamrashamra zinaendelea kwa mashabiki wapo waliopanda bodaboda,wanaotembea kwa mguu wakishangilia pembeni ya gari kubwa la wazi lililobeba wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo.

Mbali na uwepo wa gari hilo kubwa, kulikuwa na mengine ikiwemo Coaster lililoiwabeba baadhi ya maofisa wengine wa timu hiyo ya Wananchi.

Dakika tatu baada ya msafara huo kutoka uwanjani ulikwama kwa dakika 10 nje ya uwanja huo kutokana na foleni huku pikipiki mbili kubwa za Polisi wa barabarani zikisafisha njia.

Idadi ya mashabiki wa timu hiyo imekuwa ikiongezeka kadiri ambavyo msafara unajongea huku wakionekana kuufurahia ubingwa wao wa 30 ikiwa ni wa tatu mfululizo.

Wachezaji na makocha nao, hawapo nyuma kwa kuonyesha ushirikiano wa kushangilia na mashabiki wao huku beki wa timu hiyo, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ akionekana kuvalia kofia kama za kiaskari.

Kitendo cha Bacca kuvaa kofia hiyo, kimewafanya baadhi ya mashabiki, kumpigia saluti wakati msafara huo ukiendelea kuchanja mbuga.

Kila ambapo msafara unapita shughuli mbalimbali zimeonekana kusimama kwa muda ikiwemo biashara kuanzia ndogondogo hadi kubwa ili kupisha mabingwa hao wa Kihistoria.

Wapo ambao walikuwa wakifunga maduka maeneo ya Veta Chang’ombeĀ  na wengine kuondoa biashara zao ndogondogo ambazo walitandaza karibu na eneo hilo la barabara.

Wakati msafara ukiendelea baadhi ya mashabiki wameonakana wakivamia bomba la maji safi na kuanza kunywa maji bila ya ruhusa ya mwenyewe kitendo ambacho kinaonekana kuzua taharuki.

Tukio hilo limetokea Veta Chang’ombeĀ  ikiwa ni dakika 50 tu tangu kuanza kwa msafara huo wa Wananchi hata hivyo hata alipotikeza mwenye bomba hilo imebidi awatazame tu mashabiki hao.

Related Posts