WANANCHI TUNZENI MIUNDOMBINU YA BARABARA – MHE. LONDO

NA OR-TAMISEMI , SINGIDA

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa rai kwa wananchi wa kata ya Minyughe na Makilawa kuhakikisha wanatunza miundombinu ya daraja la MInyughe lililojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.8

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Denis Londo leo Mei 25,2024 wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ,Mkoani Singida

Amesema ujenzi wa daraja hilo la chuma lenye urefu wa mita 30 katika barabara ya Mtamaa- Minyughe hadi Mtavila yenye urefu wa km 27 itafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa kata hizo

Mhe. Londo amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini hivyo ni wajibu wa kila mwansnchi kuhakikisha wanatunza miundombinu inayojengwa

“Kuna baadhi ya wananchi wachache ambao si waaminifu huaribu miundombinu na wengine kuchukua kama vyuma chakavu
hili halikubaliki kila mwananchi anawajibu wa kulinda miundombinu hiyo”amesisitiza

Naye Mbunge wa Singida magharibi Elibariki Kingu ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya mendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida

Aidha, ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa Daraja la Minyughe ambalo limesaidia kupunguza kero kwa wananchi wa maeneo hayo hasa wakati wa kipindi cha mvua.

Related Posts