MSAFARA wa Paredi la Kibingwa la Yanga inayosherehekea ubingwa wa 30 katika Ligi Kuu Bara na wa misimu mitatu mfululizo haushi vituko, kwani mara ulipoibukia pembeni ya soko la bidhaa la Karume, maeneo la Ilala, beki wa kulia wa timu hiyo, Yao Kouassi alijikuta akipewa zawadi ya aina yake.
Yao akiwa kwenye furaha na mashabiki waliokuwa wamesimama kando ya barabara kikarushwa kiroba kidogo cha Nyanya kisha akakidaka kwa umakini.
Baada ya kukidaka kiroba hicho beki huyo anayejulikana kwa jina la jeshi akaanza kushangiliwa kwa nguvu huku naye akiinua juu.
Baada ya Yao kukipokea kiroba hicho akamkabidhi kinara wa mabao wa Ligi Kuu Bara Stephanie Aziz KI kisha kuanza kufurahia zawadi hiyo.
Hayo yanajiri kwenye paredi ya ubingwa wa Yanga inavyoendelea kukatiza mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam wakilitembeza komb la ubingwa wao wa Ligi Kuu