CRDB BANK YAZIFUNDA ELIMU YA FEDHA TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI PWANI

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

Benki ya CRDB tawi la Kibaha katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan  imetoa elimu ya fedha kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali zipatazo 22 za Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo.

Pia benki hiyo sambamba na hilo imeweza  kuzipa mbinu mbali mbali pamoja na  kuzishauri taasisi hizo kuweka mikakati ya  kufungua akaunti ya NIA MOJA ambayo ni akaunti mahsusi kwa vikundi na haina makato yoyote ya kila mwezi.

Hayo yamebainisha na  Meneja wa biashara wa CRDB tawi la Kibaha mjini Richard Mkakala wakati wa kikao kazi maalumu ambacho kilizikutanisha taasisi zizosokuwa za kiserikali kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali yanayohusiana na uchukuaji wa fedha na utunzaji wake kupitia mfumo wa kufungua akaunti.

Meneja huyo Mkakala alisema kwamba kwa sasa benki ya CRDB wameanzisha akauniti ya   NIA MOJA ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuweka  fedha za taasisi ili ziwe katika hali ya usalama  katika kipindi chote bila wasiwasi.

Kadhali Meneja huyo alifafanua kwamba  wanachama hasa kwa upande wa  wanawake wanashauriwa kufungua akaunti ya iMBEJU ili wazitumie katika kuweka  akiba zao na kupitisha mapato ya biashara zao mbali mbali kwa urahisi zaidi.

” Ninyi wanachama mkiwa na akaunti za CRDB, mnayo fursa kubwa zaidi  kupitia katika hizi  taasisi zenu kuweza  kunufaika na mpango wa uwezeshaji unaowalenga wanawake kuwapa mitaji midogogo kwa ajili ya kuendeleza biashara zenu ili ziweze kukua na kuwa kubwa,”alifafanua Meneja huyo.

Kadhalika aliongeza kuwa lengo lao kubwa ni kuziwezesha taasisi hizo ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa masharti nafuu ambayo wanaweza kuyamudu lengo ikiwa waweze kutimiza malengo yao waliyojiwekea.

 “Kwa kweli sisi kama benki ya CRDB kwa sasa tuna  uwezeshaji huu wa kuziwezesha taasisi mbali mbali mbali zisizokuwa za kiserikaki na kiukweli  unatolewa kwa masharti nafuu sana na benki yetu,”aliongeza Meneja huyo.

Katika hatua nyingine alizishauri na kuzihimiza taasisi zote ambazo zimesajiliwa rasmi  hiyo nazishauri  kuhakikisha zinafungua akaunti ya CRDB  ili kuwa na uhakika zaidi juu ya   usalama wa fedha zao.

 Pia aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kuhakikisha wanajiunga katika vikundi mbali mbali na kuvisajili ili viweze kutambulika na  kupata fursa ya  mikopo katika benki hiyo  kwa  masharti nafuu zaidi.

Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu mbali mbali kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali pamoja na wanachi juu ya umuhimu wa kufungua akaunti ili kuweza kutunza fedha zao zikiwa katika hali ya usalama.


Related Posts