DC Kissa awataka madereva kuwa na bima ya vyombo vyao ili kuwa na uhakika wa fidia wanapopata ajali

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amewataka maafisa usafirishaji wilayani humo kuwa wa mfano kukata bima kwa ajili ya vyombo vyao vya usafiri ili kuto weka rehani maisha yao na wanaowategemea kwa kuwa bima itakuwa msaada kwao na wanaowategemea baada ya ajali.

DC Kissa ameeleza hayo wakati akizungumza na madereva wa bajaji ambapo amewataka maafisa wasafirishaji na wafanyabiashara kukata bima ili kuwa na uhakika wa vyombo vyao au biashara yanapotokea majanga ikiwemo ajali au maduka kuungua moto.

“Ajali ni sehemu ya changamoto kwa mtu ukiwa na chombo cha moto sasa kama hatujilindi tutakuwa tumeweka maisha yetu rehani na tunaweka maisha ya wanaotutegemea rehani lakini ukiwa na bima ina kukinga wewe na ikitokea bahati mbaya umefariki wale wanaobaki watapata fidia kupitia bima”amesema Kissa

Paul Mkumbo ni Meneja wa shirika la bima la taifa (NIC) kanda ya kusini kati amesema kundi hilo ni muhimu na kutokanana umuhimu huo wameweza kuingia makubaliano ya kuwahudumia pamoja na kuwafanya madereva hao kuwa sehemu ya shirika kwa kuwapa fursa na kuhakikisha vyombo vyao vyote vina tii sheria kwa kukata bima.

“Tumeingia makubaliano nao kwa hiyo kadri watavyowafikia makundi mbalimbali katika sekta ya usafirishaji ndivyo ambavyo wao pia wataweza kujiongezea mapato”amesema Mkumbo

Nao baadhi ya madereva akiwemo Omary Mng’ong’o wanasema upo umuhimu mkubwa wa kuwa na bima ili kujiweka kwenye usalama zaidi ambapo wamepongeza NIC kwa kuweza kufikia kundi hilo.

Related Posts