EWURA YAENDESHA SEMINA KWA KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA , Bw.Msafiri Mtepa akijibu hoja wakati wa semina kuhusu ukokotoaji wa bei za bidhaa za mafuta kwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini,leo 27.5.2024, Bungeni Dodoma

……………

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo 27.5.2024 imeendesha semina ya siku moja kuhusu Ukokotoaji wa bei za bidhaa za mafuta kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Akiwasilisha mada hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Msafiri Mtepa, alisema bei za mafuta hapa nchini hupangwa kwa kutumia Kanuni ya Kupanga Bei za Mafuta ya Mwaka 2022 ambayo imekuwa ikifanyiwa marekebisho ili kuakisi mabadiliko mbalimbali yanayohusiana na upangaji wa bei za mafuta hapa nchini.

Akihitimisha semina hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Kilumbe Shaban Ng’enda (Mb) ameishukuru Wizara na EWURA kwa kuandaa semina za kuwajengea uelewa “Nawapongeza sana Wizara na EWURA kwa kuandaa semina hii kwani mmeendelea kutusaidia sisi wawakilishi wa wananchi kuwa na uelewa mpana wa sekta ya mafuta hususan umuhimu wa upangaji wa bei za bidhaa za mafuta na faida za kiuchumi kutokana na kuwa na mfumo wa uagizaji wa wa mafuta kwa pamoja” alisema

Semina hiyo pia imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (Mb), Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati, Goodluck Shirima pamoja watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na EWURA.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA , Bw.Msafiri Mtepa akijibu hoja wakati wa semina kuhusu ukokotoaji wa bei za bidhaa za mafuta kwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini,leo 27.5.2024, Bungeni Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa kwenye semina kuhusu ukokotaji wa bei za bidhaa za mafuta iliyotolewa na EWURA leo 27.5.2024, Bungeni Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mh.Kilumbe Ng’enda (Mb) akiishukuru Wizara na EWURA kwa kuandaa semina ya kuwajengea uelewa, waheshimiwa wabunge leo 27.5.2024,Bungeni Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati Mh.Judith Kapinga (Mb) akifafanua jambo wakati wa semina ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini,leo 27.5.2024,Bungeni Dodoma

Related Posts