Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

SERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi 132,611 yenye thamani ya Sh 219.7 bilioni.

Aidha, imetoa wito kwa waajiri wote nchini hususanu wakurugenzi wa halmashauri kuhakiki na kuwasilisha madeni ya watumishi kwa ajili ya taratibu za uhakiki na malipo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pia imewataka wabunge kuwaharakisha wakurugenzi hao wa halmashauri kupeleka taarifa hizo za watumishi wanaodai ili walipwe haraka kwani Serikali inayo bajeti ya kutosha kulipa madeni hayo.

Neema Mgaya

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Mgaya.

Katika swali la msingi, Mgaya alihoji ni ni lini Serikali itamaliza kulipa madeni ya muda mrefu ya watumishi.

Akiendelea kujibu maswali hayo, Kikwete amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kudhibiti uzalishaji wa madeni ya watumishi ikiwemo malimbikizo ya mishahara kwa kujenga Mfumo Mpya wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) ulioanza kutumika mwezi Mei, 2021 ambao umeweza kudhibiti uzalishaji wa malimbikizo mapya ya Mishahara.

“Lini tutamaliza madeni, kwa mujibu wa taarifa na taratibu tunataka tuwahakikishe hata leo, ila kinachotukwamisha ni waajiri ambao hawaleti taarifa kwa wakati. Serikali inatoa wito tena kwa waajiri kuhakiki na kuwasilisha taarifa ya madeni ya watumishi umma ili serikali iwalipe.,” amesema.

Related Posts