Marufuku mikopo kausha damu wilayani Mbogwe

Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Bi. Sakina Mohamed amepiga Marufuku Mikopo umiza katika wilaya yake kwa madai imekuwa haiko kisheria kutokana na Akina Mama wengi kulizwa kwa kuongezwa riba zisizokuwa na lengo la Kumnyanyua mwanamke kiuchumi.

Akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke na Samia wilayani humo Sakina amesema kumekuwepo na Kesi nyingi za Akina Mama ambazo zimekuwa zikiripotiwa juu ya mikopo hiyo ambayo imekuwa ikifahamika kwa Majina ya Kausha damu na Mikopo kichefu chefu.

“Tumeona Mabango yanapita hapo si ndio mikopo kandamiza ,Mikopo umiza kausha damu sasa nataka niseme na mara zote huwa nasema mikopo kausha damu wilaya ya Mbogwe kwisha haiwezekani nikiona kuna Mama yoyote anaumia kwa sababu ya Mkopo kausha damu njoo kwenye Ofisi ya DC tuna maliza huo Mchezo , ” DC. Sakina Mohamed.

Sakina amesema lengo la kuanzisha Taasisi hiyo katika wilaya ya Mbogwe ni kuchangia jitihada anazofanya Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kumkomboa mwanamke kiuchumi huku akipiga Marufuku wanawake kudhurumiwa haki zao kinyume na Sheria za nchi.

“Kwa sababu huyo nae nitapeli kama matapeli wengine hajaripia riba halipii serikali popote kwahiyo huyo nae anamwibia mwanamke anatumika kumgandamiza mwanamke kwa njia moja ama nyingine kwahiyo nataka niseme kama kuna Mama yoyote ambaye anakaribia kuvunja ndoa yake kwa sababu ya mikopo kandamiza njoo ofisi ya DC tumalize kazi , ” DC. Sakina Mohamed.

Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa kutoka Mkoa wa Geita , Evarist Gerevas amesema vilio na Manyanyaso kwenye utawala wa Awamu ya Sita havitokubaliwa kwani mwanamke anazo sifa za kuwa kiongozi bora .

“Hakuna sababu ya kuendelea kuwa wanyonge mwenyezi mungu amemuleta mtetezi wenu amemuleta kiongozi anayejua uchungu wa akina mama amemuleta kiongozi kwenye utayari wa kuwatumikia wakaina Mama wote wa Tanzania ikiwemo na Mbogwe hii , ” MNEC. Evaristi.

Adelina Kabakama ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Samia Mkoa wa Geita amewataka wanawake wa Mkoa wa Geita kuungana kwa pamoja katika kuchangia nguvu Kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa Mfano bora katika kuzingatia usawa katika nafasi mbalimbali za kiutendaji.

Related Posts