Marufuku wananchi kuchangia maji na wanyama

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew amezilekeza Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira mkoani Morogoro (MORUWASA), Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) pamoja na Bonde la Wami Ruvu kukamilisha miradi ya maji ili kutimiza lengo la Serikali juu ya upatikanaji wa maji kwa 95% mijini na 85% vijijini ifikapo mwaka 2025.

Amezungumza hayo katika ziara yake mkoani humo ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maji Mgulu wa ndege, mradi wa maji Sokoine na mradi wa maji ambao upo katika kijiji cha Kichangani wilayani Mvomero ambapo amesisitiza kuwa ni wakati sasa wananchi kupata maji safi na salama

Aidha, Waziri Kundo amekemea vikali suala la wananchi kutumia maji pamoja na mifugo mbadala wake kuwepo vituo vya kuchotea maji na mabirika maalumu ya kunyweshea mifugo ili kuepuka magojwa mbalimbali kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa maji safi na usafi wa mazingira MORUWASA Mhandisi Tamimu Katakweba amesema tayari wameanza kuchukua hatua kadhaa ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya maji iliyoharibiwa na mvua ili wananchi waweze kupata maji safi na salama, pia watahakikisha miradi inayoendelea katika mkoani humo inakamilika kwa wakati.

Related Posts