Mradi wa maji Same – Mwanga 90% ya utekelezaji, Aweso awasha pump kusukuma maji kwenda tenki la mwisho.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ametembelea na kukagua mradi wa maji Same Mwanga Korongwe ambao umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake ambapo ameshuhudia mifumo ya kutibu maji imekamilika na kisha akafanya zoezi la kuwasha pump za kusukuma maji kupeleka kwenye Tank kubwa la Maji la Kiverenge.

Sambamba na hilo Mhe. Aweso ametembelea pia eneo la Lembeni na kujioneo shughuli ya kuvusha bomba chini ya barabara ikiendelea ambapo ameelekeza kazi hiyo ikamilize ndani ya masaa 24 ili wananchi wapate huduma ya maji kwa haraka.

Waziri Aweso ametembelea na kukagua mwanzo hadi mwisho wa mradi ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Makamu wa Rais Mhe Dkt. Philip Mpango ya kuhakikisha mwisho wa mwezi Juni 2024 wananchi wa Same – Mwanga wanapata huduma ya uhakika ya majisafi na salama.

Waziri Aweso ameshuhudia mazingira magumu ya kazi katika kumaliza ujenzi wa Mradi na pamoja na hilo ameridhishwa na kasi na morali iliopo na amewahakikishia wana Same-Mwanga-Korogwe kazi hii itakamilika kwa wakati kama yalivotolewa Maelekezo na viongozi wakuu.

Related Posts