Naibu Waziri Mkuu Dkt.Dotto Biteko apiga marufu viongozi kuingilia Mihimili

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Dkt. Dotto Biteko amepiga marufu kwa viongozi kuingilia mihimili badala yake wawasaidie wananchi kutatua changamoto zao bila kuvunja utaratibu wa kisheria huku akitaka mihimili kufanya kazi kwa pamoja.

Biteko ametoa maelekezo hayo mkoani Njombe wakati akizindua kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campain) kwa mkoa huo.

“Nchi hii inaongozwa na katiba,serikali ina majukumu yake,Mahakama ina majukumu yake na Bunge lina majukumu yake istokee mhimili mmoja ukataka kuingilia majukumu ya muhimili mwingine badala yake mihimili yote ifanye kazi kwa nia moja ya kuwahudumia watanzania”amesema Biteko

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Biteko amesema takwimu inaonyesha mwamko mkubwa wa wanaume kwa sasa wameanza kujitokeza kueleza changamoto zao ikiwemo ukatili wanaofanyiwa kwenye jamii ili waweze kusaidiwa ukilinganisha na awali ambapo kundi la wanaume walikuwa wakikaa kimya huku wakifa na tai shingoni kutokana na changamoto wanazopitia.

Amesema tangu ilipoanza kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campain) inayosimamiwa na Wizara ya Katiba na sheria ambapo halmashauri 42,kata 452 na vijiji 1348 vimekwishafikiwa,wanaume wameonyesha kuongoza kueleza changamoto walizonazo.

“Toka mmeanza hii kampeni watu wengi mmewafikia watu 415,597 mmewasikiliza na katika watu waliofikiwa na kampeni hii wanaume ni 216,000 na wanawake ni 199,000 kwa hiyo wanaume wamenaza kujitokeza kwa wingi na bila shaka wataendelea kuja kwasababu huko nyuma pengine ilikuwa mushkeli kidogo kwa mwanume kulalamika unakufa na tai shingoni lakini baada ya kampeni wanaume wengi wameendelea kujitokeza na bila shaka wataendelea kujitokeza”Amesema Biteko

Related Posts