Usimamizi wa matumizi salama ya mtandao

Matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ni suala muhimu katika jamii ya leo inayojikita katika teknolojia.

Mitandao ya kijamii imerahisisha mawasiliano na kuwezesha watu kuungana na wengine ulimwenguni kote.

Hata hivyo, ni muhimu kuwa na mwongozo wa jinsi ya kutumia mitandao hii kwa njia yenye tija na yenye kuheshimu wengine.

Hata hivyo, ni dhahiri kuwa  tumeshuhudia maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia na sasa dunia ipo katika Mapinduzi ya kidijitali  ambayo yanaongozwa na sekta ya TEHAMA.

Kutokana na maendeleo hayo, shughuli nyingi duniani kwa sasa zinafanyika kwa kutumia TEHAMA. Hivyo, kila mmoja hana budi kuendelea kujihuisha na sera na miongozo  ili kuendana na mabadiliko hayo.

Katika jitihada za kuhakikisha huduma  zinatolewa kwa njia ya kielektroni,upo umuhimu wa uelewa na matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na data miongoni mwetu katika matumizi mbalimbali ya kimtandao.

Ingawa kompyuta, simu za mkononi na vifaa vingine vya elektroniki vyenye intaneti vimeleta nafasi nyingi za ajira, pia vimeleta changamoto na hatari nyingi ikiwemo unyanyasaji kingono ,ulaghai na hata wizi.

lakini zipo njia za kulinda taarifa zako na ukawa na matumizi bora ya mtandao:

1.Tumia uthibitishaji wa hatua mbili kwa akaunti zako

2.Unda manenosiri refu/thabiti  Hizi zinapaswa kuwa mchanganyiko wa nambari, alama na herufi na zisiwe na taarifa za kibinafsi zinazoweza kutambulika, kama vile tarehe yako ya kuzaliwa

3.usitumie nenosiri moja badala yake unda nenosiri jipya kwa kila akaunti.

4.fahamu unachokitaka kwenye mtandao na nani unataka kuwafikia

5.Toka nje ya akaunti na vifaa vyako kila mara inapowezekana.

6.Ni muhimu kutotunza taarifa zako kwenye mtandao, hasahasa vitu/taarifa binafsi kama picha kwa kuwa huwezi kudhibiti namna zinavyotumiwa.

#zainafoundation , #keepiton

Related Posts