JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limesema litaendelea kuimarisha ulinzi wa Mkoa

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limesema litaendelea kuimarisha ulinzi wa Mkoa huo ambao ndio kitovu cha utalii hapa nchini huku likibanisha kuwa leo limeendelea na utoaji elimu kwa madereva wanao pokea na kutoa huduma ya usafiri kwa wageni wanafika Mkoani humo kwa ajili kutalii.

Akiongea mara baada ya kikao hicho na wadau wa usafirishaji Mkuu wa Opersheni za Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Salvatory Makweli amesema kuwa huo ni mwendelezo wa kuweka mazingira bora na salama kwa wageni wanaokuja kutalii Mkaoni humo.

ACP Makweli amewetaka Madereva hao kutmbua kuwa kipindi hiki ndicho watalii wengi wanafika katika Mkoa huo kwa ajili ya kutalii ambapo amewataka wasafirishaji hao kuweka utambuzi wa vyombo vyao ili kuwabaini wale wanachafua taswira nzuri ya watoa huduma za usafiri kwa watalii.

Vilevile amewambia endapo watatekeleza agizo hilo watakuwa wamepunguza na kuondoa malalamiko ya wageni ambao wamekuwa wakilalamika juu ya watoa hudma hao katika jiji la Arusha.

Kwa upande wake Alex Athony ambaye ni mdau wa usafirishaji watalii licha ya kushukuru kwa elimu hiyo na kupewa uelekeo wa utoaji huduma bora kwa watalii amebainisha kuwa licha kutoa huduma hiyo amesema kuwa magari wanayotumia ni magari ambayo yanakizi viwango kwa kwa wageni na watalii.

Nae Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkao wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema kuwa kikosi hicho kimeendela kutoa elimu ili kuweka mazingira salama kwa watalii wanaofika Mkoani humo kwa ajili ya utalii huku akiwataka kuwa mabalozi wazuri ambao wataitagaza Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Related Posts