KARIBU BANDA LA NBAA JIJINI TANGA KUPATA ELIMU YA UHASIBU NA UKAGUZI

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) inaendelea kutoa elimu kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024 yanayoendelea katika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal jijii Tanga ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amefungua rasmi Maadhimisho hayo.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho hayo amesema Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ni sehemu ya mikakati ya serikali katika kuongeza hamasa ya kukuza elimu ujuzi na ubunifu katika kuchangiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi kwa mwananchi waliotembelea Banda la Bodi hiyo wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.

Afisa Uhusiano na Mawasiliano kutoka NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB walipotembelea Banda la Bodi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.

Afisa kutoka Dativa Mgweno akitoa elimu kwa wanafunzi walipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.

Maonesho yakiendelea 

Meza kuu

   

Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda alipokuwa anafungua Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, ujuzi na ubunifu mwaka 2024.

Related Posts