Uzinduzi wa kitabu cha kutawala vifaa vya muziki wafanyika leo

Baraza la Sanaa nchini limewataka Wadau wa Muziki kuzingatia mabadiliko ya Kidigitali kwenye ufanisi wa kazi kwa lengo la kutatua changamoto Katika muziki ikiwa ni pamoja na usikivu wa muziki, afya ya masikio, uharibifu wa vyombo vya muziki, pamoja na kutatua uelewa mdogo juu ya vipimo vya vifaa.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Sanaa Basata Mr. Manyaga Oden wakati wa uzinduzi wa kitabu Cha kutawala vifaa vya muziki akimwakilisha Katibu mtendaji wa basata Dkt Kidmen Mapana.

” lengo la kuzinduliwa kitabu hicho ni pamoja na kufundisha na kushauri kuhusu vifaa vya muziki na kuboresha mifumo ya sauti, tutaendelea kuwathamini wale wote wanaopambana na mabadiliko ya muziki wetu kuupeleka juu kwani inazidi kuleta faida ya muziki wetu kusogea juu” Amesema Mr Manyanga.

Related Posts