WAZIRI JAFO AWASILI KATAVI KUANZA SAFARI YA KUELEKEA WIKI YA MAZINGIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasili mjini Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya ziara ya
kikazi leo tarehe 28 Mei, 2024.

Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa chini ya Mradi wa Urejeshaji wa Uoto
wa Asili unaotekelezwa katika mikao mbalimbali nchini.

Uzinduzi huo ni sehemu ya shamrashamra za kuadhimisha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni tarehe 5 Mei, 2024.

Shughuli zitakazozinduliwa ni pamoja na josho la mifugo, banio na birika la kunyweshea mifugo maji. Pia, kutakuwa na shughuli za kugawa hati miliki za
ardhi za kimila 4450 pamoja na hati ya msitu.

Mikoa ambayo mradi huo unatekelezwa Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa na Katavi katika wilaya saba.
Waziri Jafo aliyeambatana na viongozi na watalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais amepokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Bw. Albert
Msovela.

Related Posts