*Abainisha kuwa na bajeti ya vifaa hivyo kwenda kusaidia wanafunzi shuleni
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Tanga
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa kifaa kilichobuniwa na Chuo Cha VETA Kigoma cha kuongeza usikivu ni msaada mkubwa kwa Serikali kutokana na baadhi ya wanafunzi wanachangamoto ya usikivu hivyo sasa ni wakati mwafaka wa kutengeneza kwa kuwekeza bajeti yake.
Profesa Mkenda aliyasema hayo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea Mjini Tanga.
Profesa Mkenda amesema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kuwa na vifaa hivyo kutokana na Ubunifu uliofanywa inakwenda kuwaweka salama wanafunzi Wetu.
Amesema wakati mwingine mwanafunzi anafundishwa au kuambiwa haelewi kumbe anakuwa na tatizo la usikivu.
Hata hivyo amesema Ubunifu uendelee kuboreshwa na kuwa kifaa cha urahisi wa kuweka masikioni au sehemu yeyote ya mwili.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Antony Kasore amesema kuwa wanakwenda kuboresha zaidi kifaa hicho.
Aidha amesema kuwa kifaa hicho kwa Teknolojia iliyopo na Ubunifu wa Walimu wa VETA kazi hiyo inakwenda kukamilika.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa VETA Dora Tesha wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea Mjini Tanga.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza katika Banda la VETA katika Maonesho ya Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea Mjini Tanga