Chuo cha KAM chasema sekta ya afya ajira nje nje kwa wahitimu

Wanafunzi wa chuo cha KAM Kimara Korogwe wakiwa kwenye maabara

Mwanafunzi wa Chuo cha Afya vha Kam  akielezea kuhusu maabara yao kwa wageni waliotembelea chuo hicho



Wanafunzi wakiwa darasani


Sehemu ya majengo ya KAM College


Wanafunzi wa chuo cha KAM Kimara Korogwe wakiwa kwenye maabara

Na Mwandishi Wetu

CHUO cha Afya cha KAM College kilichopo Kimara jijini Dar es salaam ambacho kimebobea kwenye mafunzo ya sekta ya afya, kimepongeza juhudi za serikali katika kuwekeza kwenye miundombinu bora ya sekta ya afya 

Pongezi hizo zimetolewa leo Mei 29, 2024 na Mkurugenzi wa Chuo hicho, Dkt. Kandore Musika wakati akizungumza kuhusu  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi NACTIVET kuruhusu kuanza kwa udahili kwa wanafunzi wa mwaka wa masomo wa 2024/2025.

Wanafunzi wanaodahiliwa ni wa ngazi ya Astashahada na Stashahada katika  kozi zote zinazosimamiwa na baraza la NACTIVET.

Amesema miundombinu ya afya imesaidia kwa kiwango kikubwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi hivyo kusaidia kupata matibabu badala ya kwenda umbali mrefu.

Amesema serikali imejitahidi kuzipa vifaa vya kisasa hospitali za wilaya na mikoa kama MRI na CT SCAN ambayo vimekuwa mkombozi kwa wananchi ambao walikuwa wakipata shida kuvifuata hospitali za mbali.

“Pia tunaishukuru NACTIVET na Wizara ya Elimu kwa kufungua udahili nasisi KAM tunawakaribisha wanafunzi wanaotaka kusomea Astashahada na Stashahada katika fani za utabibu,  maabara, ukunga, meno, rekodi za afya, sayansi ya fya ya mazingirana famasia na kozi za VETA,” alisema Dk Kandore

Dkt. Kandore amesema chuo cha KAM kimekuwa kikitoa mafunzo kwa vitendo zaidi hali ambayo inawawezesha wanafunzi wanaohitimu kwenye chuo hicho kupata ajira kwa urahisi kwenye maeneo mbalimbali.

“Kutokana na kuwa na ujuzi kamili wahitimu wetu wengi hawahangaiki kutafuta ajira kwasababu wanaajiriwa na serikali na sekta binafsi, sekta ya afya bado inamahitaji makubwa ya watumishi kwa hiyo wakihitimu tu wanachukuliwa na serikali na sekta binafsi,” amesema Dkt.Musika.

“Tunawaomba wanafunzi wachangamkie fursa ya kufunguliwa na udahili ili waje wapate mafunzo ambayo yatawapatia ajira kwa urahisi na kwa anayetaka kujiunga nasisi aingie kwenye kamcollegeofhealthsciences.ac.tz.”

Amesema KAM imejiimarisha vizuri kwa kuwa na kozinyingi na hospitali yenye hadhi ya Wilaya ambao hutumika kwa wanafunzi kufanya kwa vitendo zaidi wanapokuwa masomo yao chuoni hapo.

“Chuo cha KAM ni chuo cha kwanza binafsi nchini na kinauzoefu wa kutosha tunaomba wanafunzi wajitokeze kujiunga kwasababu Wizara imeshatoa kibali cha kuendelea na mafunzo kwa vigezo vilivyokuwepo na wanafunzi wanaotaka waje chuoni Kimara Korogwe,” amesema 

“Tunamshukuru sana Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amekuwa karibu sana na vyuo binafsi vya afya nasisi tunamuahidi kwamba tutaendelea kufuata miongozo inayotolewa na wizara yake hasa kuhusu mitaala na namna yaa kuendesha haya mafunzo,” alisema

Related Posts