Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Nape Nnauye na Rais wa Taasisi ya Internet Society Tanzania Chapter(ISOC-TZ) Nazar Kilama wakipokea tuzo y a Access to Information and Knowledge ambapo ISOC -Tanzania imekuwa ya kwanza kati ya project 1049 kwenye kundi la tatu.
Picha pamoja Waziri wa Habari,. Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye baada ya kupokea Tuzo
Picha za Matukio mbalimbali wakati mkutano na upokeaji Tuzo nchini Uswis Geneva.
Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya internet Society Tanzania Chapter(ISOC-TZ)imeibuka kidedea baada ya usaili wa project 1049 toka pande za dunia baada ya usaili wa project 369 zilizoiingia kwenye kinyang’anyiro.
ISOC-Tz imeibuka kidedea kwa kuwakilisha project yao ijulikanayo kama TANZANIA DIGITAL INCLUSION PROJECT inayotekelezwa katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar Es Salaam.
Tuzo hizo zilizofanyika Geneva nchini Uswiss zinazojulikana kama World Summit on Information Society (WSIS 2024 PRIZES) ISOC -TZ ilifanikiwa kupitia hatua ya kwanza na ya pili.
Hayo ameyasema Rais ISOC Tanzania Nazar Kirama wa baada ya usaili wa mradi wa matumizi ya Internet usio na mipaka ‘Tanzania DIgital Inculusion’ nchini Uswis Geneva.
Amesema jumla ya projects zilizosailiwa zilikuwa 1049 toka pande zote za Dunia.
Aidha amesema Baada ya usaili project 360 tu ndio ambazo zimeingia kwenye kinyang’anyiro. Project yetu ni kati ya hizo project 360 ambazo ndizo wagombea wa TUZO ZA WSIS 2024.
Tuzo hiyo imepokelewa na wa Rais Wa ISOC Tanzania aliyeongozana na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kwa pamoja walishukuru Watanzania wote kwa ushirikiano walionyesha kwani hakuna mtu atae achwa nyuma.
“Naamini tuzo hii kwa Tanzania utakuwa ni mwanzo mzuri kwani hakuna mtu atae achwa nyuma tutaenda moja kwa moja kwani kama ushirikiono tuliuweza kuonyesha” alisema Kirama na kuongeza Nashukuru kwa kuwa nimeweza kupokea tuzo hii pamoja na Waziri wa wizara husika ni imaani kubwa sana kwamba Tanzania tutaendelea kufanya vizuri zaidi