*Ugunduzi umetokana na yeye mwenyewe kuwa na changamoto ya usikivu hafifu
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV Tanga
MWALIMU wa VETA Kigoma Innocent Maziku agundua kifaa cha kuongeza usikivu kutokana na yeye mwenyewe kuwa na usikivu hafifu.
Maziku amebainisha hayo katika Banda la VETA katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu ya Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea katika Viwanja Vya Shule ya Popatlal Mjini Tanga.
Amesema kuwa wakati anasoma aligundua ana changamoto ya usikivu hafifu hali hiyo ilifanya kuwa na wakati mgumu wa kusoma kwake hususani katika kumsikiliza mwalimu.
Amesema kidato cha kwanza hadi cha nne akafaulu kwenda kidato cha tano na sita akafaulu kwenda Chuo huku hiyo hali anayo ya usikivu.
Maziku amesema wakati amepata ajira ya Ualimu Kigoma baada ya muda akaanza kubuni kifaa cha kuongeza usikivu kwa mara ya kwanza hakufanikiwa lakini mara ya pili aliongeza mashine za kuongeza wawimbi ya sauti ‘Microphone’ manne na alivyojaribu akauna anapata usikivu vizuri.
Amesema katika mazingira hayo alitokea mwingine mwenye changamoto hiyo ya usikivu hafifu alivyoweka nae akawa anasikia.
Amesema kwa hatua hiyo kifaa hicho anatumia mwenyewe huku akijua wapo baadhi ya watu wanachangamoto hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa kilichobaki ni baadhi ya taasisi kuweza kupima ubora na ndipo kazi yake atengeneze kwa ajili ya kusaidia jamii.
Maziku amesema kuwa na ubunifu ambao unakuwa hauendelezwi unafanya jamii kubaki na changamoto zile zile.