UJENZI wa Vivuko vya alama za pundamilia na njia za watembea kwa miguu katika Shule za Msingi Makorora na Azimio Jijini Tanga, vimewaepusha wanafunzi kuepukana na ajali ambazo zimekuwa zikichangia vifo na majeraha mbalimbali kwao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga …(endelea).
Ujenzi huo umewezeshwa na Shirika la Amend Tanzania kupitia mradi wake Miundombinu Salama ya Barabara katika shule hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania, Saimon Kalolo alisema mradi huo umehusisha ujenzi wa njia za watembea kwa miguu, vivuko vinne vya pundamilia, matuta saba ya kupunguza mwendo kasi, alama 15 za barabarani, na michoro 16 ya usalama barabarani.
Alisema wametoa elimu ya usalama barabarani kwa jumla ya wanafunzi 1,694 na walimu wa shule za msingi Makorora na Azimio ndani ya mwezi tano, 2024 Tanga na Tanzania kwa ujumla”Alisema
Kalolo alisema katika miaka ya hivi karibuni wamepiga hatua katika kuboresha usalama barabarani kwa watoto kwa kutoa miundombinu salama na elimu.
Hata hivyo, alisema bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha usalama wa watoto wote wa Kitanzania katika safari zao za kila siku za kwenda na kurudi shuleni.
“Tukio la leo linaonyesha kuwa hatua zisizo na gharama kubwa na rahisi za kuokoa maisha zinaweza kutekelezwa kwa urahisi,”alisema.
Aliongeza kuwa mpango wa kuboresha miundombinu salama ya watembea kwa miguu ni sehemu ya mradi wa mwaka mmoja unaoitwa “Usalama wa Pikipiki kwa Vijana Tanzania”.
Alisisisitiza mradi huo unaungwa mkono na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na una bajeti ya Sh. 424,983,396 (Faranga za Uswisi 150,000).
Alieleza tokea Septemba mwaka 2023, shughuli nyingine za mradi zimejumuisha mafunzo ya waendesha pikipiki (bodaboda) 300 ndani ya Jiji la Tanga, waendesha pikipiki 253 mkoani Dodoma, kampeni ya uhamasishaji kuhusu masuala ya usalama wa pikipiki, na kuanzishwa kwa ‘Kanuni za Maadili’ kwa madereva.
Amesemw waendesha pikipiki 200 zaidi watapewa mafunzo jijini Tanga ifikapo Juni 2024 na tathmini ya athari za shughuli hizo zote inafanywa hivi sasa.
“Balozi wa Uswisi, Didier Chassot ajali za barabarani ndiyo chanzo kikuu cha vifo vya watoto na vijana wenye umri kati ya miaka 5 na 29 duniani kote nchini Tanzania na kuna zaidi ya majeruhi 330,000 wa ajali za barabarani kwa mwaka ambayo ni ya juu kuliko wastani katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara”Alisema
Alisema hilo ni tatizo kubwa la afya ya umma Uswisi linaunga mkono mpango huu kwa lengo la kuboresha usalama na kuhakikisha za kiafya kwa watumiaji wote wa barabara, hasa watoto na waendesha pikipiki vijana.
Alisema mradi huo wa kuokoa maisha unaonesha ajali za barabarani zinaweza kuzuilika kazi hiyo iliyoungwa mkono na Fondation Botnar na sasa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania, itaendelea kupunguza ajali za barabarani na kuokoa maisha.
Mkurugenzi Mkazi huyo alisema kupitia Mpango Kazi wao wa Usafiri Salama na Endelevu kwa Jiji la Tanga, wanalenga kuhakikisha kuwa kila mtoto wa Tanga anakuwa na safari salama ya kwenda na kurudi shuleni – lengo liweze kutimia kabisa.