[8:37 PM, 5/30/2024] Chalila Tg: AKU yataka vijana kujiunga katika shahada ya Uuguzi
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Tanga
CHUO Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) kimesema kuwa vijana kutumia fursa ya kujiunga na na Chuo Kikuu cha Aga Khan kusoma shahada ya kwanza ya Uuguzi kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita kwa mwaka wa Masomo 2024/2025
Akizungumza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu ,Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea katika Viwanja Vya Shule ya Sekondari Popatlal Mjini Tanga Msajili Msaidizi wa AKU Agatha Damasi amsema kuwa kozi ya shahada ya kwanza ambayo imeenza mwaka Jana.
Amesema kuwa AKU inatoa shahada zingine ambazo ni shahada ya Uuguzi kwa wafanyakazi wa sekta ya afya walioko kazini ikiwa ilenga katika kujenga uwezo kwa watoa huduma wakiwa kazini na kuendelea kusoma.
Agatha amesema kuwa kulingana kuwepo kwa mahitaji makubwa ya sekta ya afya kwa wauguzi ndipo waliamua kuanza na kozi ya shahada ya Uuguzi kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita kwa viwango vya ufaulu vilivyoanishwa na TCU.
Aidha amesema kuwa Chuo kimejipanga katika kutoa elimu ya Uuguzi kwa viwango vinavyohitajika na Shirika la Afya Duniani (WHO) ili wakihitimu kwenda kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Hata hivyo amesema kuwa AKU imejiimarisha kwa upande wa wahadhiri madaktari na Profesa katika kufundisha wanafunzi wataoanza kozi hiyo.
Amesema kuwa shahada hiyo ya Uuguzi itajikita katika ujuzi zaidi kuliko ya nadharia ambayo itamsaidia mwanafunzi kuwa sehemu ya kutatua changamoto pale atapohitimu na kwenda kutumikia kazi yake.
Amesema kuwa AKU katika uimarishaji wake wameweka maabara ya kiisasa ya kufundishia pamoja na vitendea kazi vingine ikiwa ni kuwasaidia wanafunzi watapohitimu kuwa ujuzi wa vifaa vya maabara.
Ameongezea pia ukiacha shahada za uuguzi AKU pia inatoa shaada ya uzamili ya Udaktari na elimu.
Katika Maadhimisho Agatha amewataka wazazi na wanafunzi kutembelea banda la Chuo Kikuu cha Aga Khan kupata elimu ya kozi wanazozitoa na kufanya uchaguzi.
Msajili Msaidizi wa AKU Agatha Damasi akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu , Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea katika Viwanja Vya Shule ya Sekondari ya Popatlal Mjini Tanga.
Matukio mbalimbali yanayoendelea katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ubunifu na Ujuzi kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal Mjini Tanga.