Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi wa Jumuiya ya Shia Tanzania kumpongeza kwa kazi nzuri anazozifanya kuwaletea maendeleo makubwa wananchi wa Zanzibar.
Rais Dk.Mwinyi ametoa shukrani hizo alipokutana na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania, Maulana Sheikh Hemedi Jalala na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe: 30 Mei 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameiomba Jumuiya hiyo kuendelea kuiomba Dua nchi kuidumisha katika amani na utulivu.
Rais Dk.Mwinyi amewashukuru kwa kuja kumpa pole kufuatia kifo cha Baba yake mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Naye, Sheikh Jalala amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kazi nzuri ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo huduma za jamii , miundombinu nakadhalika pamoja na kuidumisha nchi katika hali ya amani, utulivu, umoja , na mshikamano.