Mkuu wa Wilaya ya Lushoto; Niko Tayari Kushirikiana na VETA

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Japhari Kubecha akizungumza na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa VETA Dora Tesha wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal Mjini Tanga.  

Na Chalila Kibuda,Tanga

MKUU wa Wilaya ya Lushoto Japhari Kubecha amesema kuwa kama Serikali wako tayari kuwa bega kwa bega na VETA katika kuhakikisha vijana wanapata ujuzi.

Mkuu Wilaya Kubecha aliyasema hayo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu ,Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea katika Viwanja Vya Shule ya Sekondari Popatlal Mjini Tanga.

Amesema katika maendeleo ya viwanda vijana wanafursa ya kupata Ujuzi wakelwenda kuutumia kutokana na Serikali ya Awamu ya Sita kuweka mazingira katika Uwekezaji nchini.

Aidha amesema kama Serikali watahamasisha vijana kwenda kusoma fani mbalimbali katika vyuo Vya VETA ikiwemo Wilaya ya Lushoto.

Hata hivyo amesema kazi kuwa katika mazingira yaliyowekwa na vyuo Vya VETA wakati umefika wa vijana kupata ujuzi.

Related Posts