NBC Dodoma Marathon msimu wa tano kufanyika Julai 28

Benki ya NBC imezindua rasmi msimu wa tano wa mbio zake zinazofahamika kama NBC Dodoma Marathon msimu wa nne  zinazotarajiwa kufanyika tarehe 28 Julai mwaka huu jijijni Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Lengo kuu la mbio hizo ni kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na  kutoa ufadhili wa elimu kwa wanafunzi wanaosomea taaluma ya ukunga  ili kuboresha afya ya mama wa mtoto.

Hafla ya uzinduzi wa mbio hizo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha wadau mbalimbali wa mbio hizo wakiwemo wawakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Benjamin Mkapa, wadau wa habari pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi.

Hafla ya uzinduzi wa mbio hizo imefanyika leo Alhamisi jijini Dar es Salaam ikihusisha wadau mbalimbali wa mbio hizo wakiwemo wawakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Benjamin Mkapa, wadau wa habari pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Barnabas alisema kuelekea msimu wa tano wa mbio hizo benki hiyo inajivunia mafanikio makubwa iliyoyapata misimu iliyopita ikiwemo makusanyo ya zaidi ya Sh.700 milioni ambapo kati yake mil 600 zilizoelekezwa katika mapambano ya dhidi ya Saratani ya shingo ya kizazi kupitia ORCI na ufadhili wa masomo kwa wakunga 100 kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin Mkapa.

“Zaidi tumeweza kuchangia ukuaji wa mchezo wa riadha nchini ambapo kwa kushirikiana na wadau wetu mbalimbali, tumeweza kukusanya zaidi ya wakimbiaji 12,500 na hivyo kuongeza hamasa kwa mchezo wa raidha nchini, tumekuwa tukichangia kuchochea utalii na uchumi wa Mji Mkuu wa Dodoma kupitia idadi kubwa ya washiriki wanaoenda kwa ajili yakushiriki mbio hizi na pia tumewa kuzalisha vipato na ajira kwa vijana ambapo mpaka sasa tumetoa zaidi ya Sh 274 milioni kama zawadi kwa washindi na hivyo kuchangia vipato vya familia,’’ alibainisha.

Akifafanua zaidi kuhusu maandalizi ya mbio hizo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Tasiana Masimba alisema katika msimu wa tano wa mbio hizo benki hiyo imejipanga kuvutia washiriki 8,000 kutoka 5,000 walioshiriki msimu uliopita lengo likiwa ni kukusanya fedha kiasi cha Sh 300 milioni ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

“Kupitia misimu iliyopita tayari tumefanikiwa kufadhili vipimo vya saratani (screening) ya wanawake 40,000 ambapo kati yao 1,600 waligundulika kuwa na vimelea vya saratani na wakaanza matibabu mapema. Kwa upande wa wakunga tunalenga kusomesha wakunga 500 ifikapo mwaka 2028 ambapo tayari 100 tumeanza nao msimu uliopita wa mbio hizi.Tunachoomba tu watanzania waendelee kutuunga mkono kwenye jitihada hizi muhimu kwa kujisajili kwa wingi,’’ alisema Tasiana.

Aidha, Tasiana aliwashukuru wadau, mashirika na makampuni mbali mbali wakiwemo Sanlam Insurance ambao ni wafadhili wakuu wa mbio hizo huku wadau wengine wakiwa ni Jubilee Allianz General Insurance,Wasafi Media, Garda World, Metropolitan, SGA,SBC, Benki za CRDB na NMB, Computech Solutions na Hans-Paul.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Shirikisho la Riadha Taifa (RT), William Kallaghe alisema tayari wanariadha mashuhuri nchini na nje ya nchi wamethibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo za kimataifa  huku akibainisha kuwa tayari mbio hizo zimeingizwa kwenye kalenda ya matukio makubwa ya riadha duniani  ikifahamika kama mbio za kimataifa hatua ambayo itavutia zaidi washiriki kutoka nje ya nchini.

“Zaidi nitoe wito kwa waandaaji wa mbio hizi kushirikiana na Bodi ya Utalii nchini ili kushirikiana kwa pamoja kutokana na ukweli kwamba mbio hizi kwasasa zina mchango mkubwa katika kuchochea utalii wa ndani,’’ alisema Kallaghe.

Kwa upande wake, Muwakilishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road  (ORCI), Dk. Crispin kihesa,alisema kupitia mbio hizo taasisi hiyo imejipanga kuendelea kutoa elimu zaidi ya saratani ya shingo ya kizazi  ili kuimarisha afya ya mama na mtoto  nchini, huku akibainisha kuwa kiasi cha Sh 600 milioni kilichokusanywa kupitia mbio hizo kimeokoa fedha kiasi cha Sh billioni mbili ambayo ingetumiwa na wahanga wa changamoto ya saratani ya kizazi endapo wangechelewa kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu mapema.

“Kupitia mbio hizi za NBC Dodoma Marathon tumeweza kunufaika zaidi kupitia ufadhili unaotuwezesha kufanya vipimo vya kutambua saratabi (Screening) kwa wanawake wengi zaidi na hivyo tumewaza kubaini tatizo hili katika hatua ya awali kabisa  na kuokoa maisha yao. Zaidi kupitia jukwaa la mbio hizi tumekuwa tukipata fursa ya kutoa kuhusu saratani ya shingo ya uzazi jambo ambalo ni muhimu zaidi,’’ alisema.

Kwa Upande wake Muwakilishi wa taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Remmy Moshi aliishukuru benki hiyo kwa ushirikiano huo unaoisaidia taasisi hiyo kufanikisha upatikanaji wa fedha zitakazosaidia kusomesha wakunga zaidi  na kuboresha huduma ya afya kwa mama na mtoto.

“Tatizo la uhaba wa wakunga bado ni kubwa tunawashukuru Benki ya NBC kwa kutuunga mkono kwenye hili na tunawasihi watanzania kujumuika katika mbio hizi ili kuokoa maisha ya wakina mama na watoto,’’ alisema.

Usajili wa mbio za NBC Dodoma Marathon umefunguliwa rasmi hivyo washiriki wanaweza kujisajili kupitia tovuti ya www.events.nbc.co.tz na kuchangia kiasi cha Sh 35,000 kwa usajili wa mtu mmoja mmoja au 25,000 kwa usajili wa kikundi chenye idadi ya watu wanaozidi 25.

Related Posts