Ninja amalizana na Lubumbashi Sport, ofa mpya hizi hapa

OLIPA ASSA
MWANASPOTI limepata taarifa za beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kupelekewa ofa na klabu za ndani ya DR Congo kama TP Mazembe, AS Vita, FC Lupopo, baada ya kuachana rasmi na Lubumbashi Sport.

Baada ya taarifa hizo alitafutwa Ninja ili kutoa ufafanuzi kama kuna ukweli juu ya hilo, alisema: “Nina barua ya kumalizana na klabu ya Lubumbashi Sport, ingawa katika hilo siwezi kuzungumza sana.”

Kuhusiana na timu anazohusishwa nazo, alisema ana ofa kadhaa zikiwemo na timu za Tanzania, ila kwa sasa anaona apate muda wa kupumzika baada ya kutoka kumaliza msimu.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

“Jamani wachezaji tuna familia, kuna muda ukitoka kwenye majukumu lazima utahitaji kukaa na mke, ndugu na jamaa, ingawa natambua soka ni kazi yangu, hivyo najipa muda kuona ofa gani itanifaa.

“Kabla sijarejea Tanzania zipo timu nilifanya nazo mazungumzo, ila sijafikia nazo mwafaka, kuhusu timu za Tanzania bado ni mapema, ukifika muda mtajua tu.”

Ninja alijiunga na klabu hiyo, akitokea Yanga ambako alicheza kwa nyakati tofauti 2017-2019 akapata dili ya kusajiliwa na MFK Vyskov iliyompeleka kwa mkopo LA Galaxy ya Ligi Kuu ya Marekani, kisha akavunja mkataba na kurejea Yanga 2020 hadi 2023 ilipoachana naye.

Related Posts