Mwalimu wa VETA Kipawa Ricky Sambo akizungumza na Wanafunzi wa Sekondari Waliotembelea Banda la VETA katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu,Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Popatlal Mjini Tanga.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MWALIMU VETA Kipawa Ricky Sambo amesema kuwa vijana wamewekewa mazingira rafiki ya fursa ya ajira katika fani ya Mechatronics kutokana mahitaji yaliyoko katika Sekta ya viwanda.
Mwalimu Sambo amesema hayo katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea katika Viwanja Vya Shule ya Sekondari Popatlal Mjini Tanga.
Amesema Sekta ya viwanda inakua nchini hivyo kunahitaji vijana wenye Ujuzi wa kuweza kuhudumia viwanda hivyo na sio kuhitaji wataalam kutoka nje ya nchi.
Amesema kuwa kozi hiyo inatolewa katika Chuo cha VETA Kipawa ambapo wanahitaji vijana kwenda kusoma ili kusaidia viwanda vilivyopo nchini na vinaendelea kujengwa.
Amesisitiza kwamba mafundi na wataalamu walioko viwandani hivi sasa wanaweza kuongeza ujuzi wao kupitia mafunzo hayo ili kuongeza ufanisi kwenye uzalishaji na huduma za usafirishaji na nyanja yoyote inayohitaji kuendesha mifumo ya automesheni.
Aidha amesema kuwa vijana wakisoma Mechatronics wanaweza kujiajiri kutokana na uwepo soko kubwa ya uhitaji wa wataalam.
Amesema katika Maadhimisho hayo vijana wafike katika Banda la VETA kujionea ujuzi unaofanywa na vijana katika fani ya Mechatronics.
Aidha amesema fani hiyo kadri ya siku zinavyokwenda mbele mabadiliko ya Teknolojia yanakua makubwa zaidi ambapo vijana wakipata ujuzi wanakuwa msaada kwa Taifa .