Benki ya NBC Yazindua Rasmi Msimu wa Tano wa Mbio za NBC Dodoma Marathon.

Benki ya NBC imezindua rasmi msimu wa tano wa mbio zake zinazofahamika kama NBC Dodoma Marathon msimu wa nne zinazotarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu jijijni Dodoma.

Lengo kuu la mbio hizo ni kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wanafunzi wanaosomea taaluma ya ukunga ili kuboresha afya ya mama wa mtoto.

Hafla ya uzinduzi wa mbio hizo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha wadau mbalimbali wa mbio hizo wakiwemo wawakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Benjamin Mkapa, wadau wa habari pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Barnabas alisema kuelekea msimu wa tano wa mbio hizo benki hiyo inajivunia mafanikio makubwa iliyoyapata misimu iliyopita ikiwemo makusanyo ya zaidi ya Sh.700 milioni ambapo kati yake mil 600 zilizoelekezwa katika mapambano ya dhidi ya Saratani ya shingo ya kizazi kupitia ORCI na ufadhili wa masomo kwa wakunga 100 kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin Mkapa.

“Zaidi tumeweza kuchangia ukuaji wa mchezo wa riadha nchini ambapo kwa kushirikiana na wadau wetu mbalimbali, tumeweza kukusanya zaidi ya wakimbiaji 12,500 na hivyo kuongeza hamasa kwa mchezo wa raidha nchini, tumekuwa tukichangia kuchochea utalii na uchumi wa Mji Mkuu wa Dodoma kupitia idadi kubwa ya washiriki wanaoenda kwa ajili yakushiriki mbio hizi na pia tumewa kuzalisha vipato na ajira kwa vijana ambapo mpaka sasa tumetoa zaidi ya TZS milioni 274 kama zawadi kwa washindi na hivyo kuchangia vipato vya familia.’’ Alibainisha.

Akifafanua zaidi kuhusu maandalizi ya mbio hizo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Bi. Tasiana Masimba alisema katika msimu wa tano wa mbio hizo benki hiyo imejipanga kuvutia washiriki 8,000 kutoka 5,000 walioshiriki msimu uliopita lengo likiwa ni kukusanya fedha kiasi cha sh mil 300 ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

“Kupitia misimu iliyopita tayari tumefanikiwa kufadhili vipimo vya saratani (screening) ya wanawake 40,000 ambapo kati yao1,600 waligundulika kuwa na vimelea vya saratani na wakaanza matibabu mapema. Kwa upande wa wakunga tunalenga kusomesha wakunga 500 ifikapo mwaka 2028 ambapo tayari 100 tumeanza nao msimu uliopita wa mbio hizi.Tunachoomba tu watanzania waendelee kutuunga mkono kwenye jitihada hizi muhimu kwa kujisajili kwa wingi,’’ alisema Bi Tasiana.

Aidha Bi Tasiana aliwashukuru wadau, mashirika na makampuni mbali mbali wakiwemo Sanlam Insurance ambao ni wafadhili wakuu wa mbio hizo huku wadau wengine wakiwa ni Jubilee Allianz General Insurance,Wasafi Media, Garda World, Metropolitan, SGA,SBC, Benki za CRDB na NMB, Computech Solutions na Hans-Paul.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Shirikisho la Riadha Taifa (RT) Bw William Kallaghe alisema tayari wanariadha mashuhuri nchini na nje ya nchi wamethibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo za kimataifa huku akibainisha kuwa tayari mbio hizo zimeingizwa kwenye kalenda ya matukio makubwa ya riadha duniani ikifahamika kama mbio za kimataifa hatua ambayo itavutia zaidi washiriki kutoka nje ya nchini.

“Zaidi nitoe wito kwa waandaaji wa mbio hizi kushirikiana na Bodi ya Utalii nchini ili kushirikiana kwa pamoja kutokana na ukweli kwamba mbio hizi kwasasa zina mchango mkubwa katika kuchochea utalii wa ndani,’’ alisema Kallaghe.

Kwa upande wake, Muwakilishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dkt. Crispin kihesa,alisema kupitia mbio hizo taasisi hiyo imejipanga kuendelea kutoa elimu zaidi ya saratani ya shingo ya kizazi ili kuimarisha afya ya mama na mtoto nchini, huku akibainisha kuwa kiasi cha sh mil 600 kilichokusanywa kupitia mbio hizo kimeokoa fedha kiasi cha sh bil 2 ambayo ingetumiwa na wahanga wa changamoto ya saratani ya kizazi endapo wangechelewa kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu mapema.

“Kupitia mbio hizi za NBC Dodoma Marathon tumeweza kunufaika zaidi kupitia ufadhili unaotuwezesha kufanya vipimo vya kutambua saratabi (Screening) kwa wanawake wengi zaidi na hivyo tumewaza kubaini tatizo hili katika hatua ya awali kabisa na kuokoa maisha yao. Zaidi kupitia jukwaa la mbio hizi tumekuwa tukipata fursa ya kutoa kuhusu saratani ya shingo ya uzazi jambo ambalo ni muhimu zaidi,’’ alisema.

Kwa Upande wake Muwakilishi wa taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation Remmy Moshi aliishukuru benki hiyo kwa ushirikiano huo unaoisaidia taasisi hiyo kufanikisha upatikanaji wa fedha zitakazosaidia kusomesha wakunga zaidi na kuboresha huduma ya afya kwa mama na mtoto.

“Tatizo la uhaba wa wakunga bado ni kubwa tunawashukuru Benki ya NBC kwa kutuunga mkono kwenye hili na tunawasihi watanzania kujumuika katika mbio hizi ili kuokoa maisha ya wakina mama na watoto,’’ alisema.

Usajili wa mbio za NBC Dodoma Marathon umefunguliwa rasmi hivyo washiriki wanaweza kujisajili kupitia tovuti ya www.events.nbc.co.tz na kuchangia kiasi cha TZS 35,000 kwa usajili wa mtu mmoja mmoja au 25,000 kwa usajili wa kikundi chenye idadi ya watu wanaozidi 25.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas (wa pili kushoto)
sambamba
Makamu wa Rais
Shirikisho la Riadha Taifa (RT) Bw William Kallaghe

(wa pili kulia), Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Insurance Bw Mika
Samwel (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio za NBC Marathon
Bi  Tasiana Masimba (kulia) wakijipongeza
kwa uzinduzi wa msimu wa tano wa mbio za NBC Dodoma marathon zinazotarajiwa
kufanyika jijini Dodoma Julai 28 mwaka huu.Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo
jijini Dar es Salaam.

Hafla ya uzinduzi wa mbio hizo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha wadau mbalimbali wa mbio hizo wakiwemo wawakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Benjamin Mkapa, wadau wa habari pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi.

Msanii Mzee wa Bwax alikuwepo kutoa burudani wakati wa uzinduzi huo.

Hafla ya uzinduzi wa mbio hizo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha wadau mbalimbali wa mbio hizo wakiwemo wawakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Benjamin Mkapa, wadau wa habari pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi.

Mdau wa habari kutoka Wasafi Media, Bw Maulid Kitenge (Kushoto) akizungumza kuhusu mkakati wa chombo hicho cha habari katika kuinadi mbio hiyo. 

Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki ya NBC Bw David Raymond (wa pili kulia) akizungumza kuhusu mbio hizo wakati wa uzinduzi huo.

Mkuu wa Idara ya Mahusianoa na Mawasiliano wa Benki ya NBC Bw Godwin Semunyu (alieshika mic) akiongoza mjadala wakati wa uzinduzi huo.

Akifafanua zaidi kuhusu maandalizi ya mbio hizo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Bi. Tasiana Masimba (katikati) alisema katika msimu wa tano wa mbio hizo benki hiyo imejipanga kuvutia washiriki 8,000 kutoka 5,000 walioshiriki msimu uliopita lengo likiwa ni kukusanya fedha kiasi cha sh mil 300 ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

Related Posts