Morogoro. Chama cha Demockasia na Maenendeo (Chadema) Jimbo la Morogoro mjini leo Mei 31, kinafanya uchaguzi wa viongozi wa jimbo na wa mabaraza matatu ya chama hicho kwa miaka mitano ijayo.
Mabaraza hayo yanayofanya uchaguzi ni Baraza la vijana (Bavicha), Baraza la Wazee (Bazesha) na Baraza la Wanawake (Bawacha).
Mjumbe wa Kamati Kuu na Kamanda wa operesheni Kanda ya Kati, Patrick Ole Sosopi amesema kuwa uchaguzi huo unaofanyia katika Ukumbi wa Double M, pia utawachagua wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa.
“Uchaguzi huu unafanywa baada ya kukamilisha ratiba ya uchaguzi ngazi ya msingi, tawi na kata na baada ya uchaguzi huu tutapata viongozi watakaokuwa wajumbe katika mkutano mkuu wa mkoa na kanda,” amesema Ole Sosopi.