DKT NCHEMBA AZINDUA MFUMO WA KIELETRONIKI WA FORODHA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCTIFI) uliofanyika tarehe 31 Mei, 2024, katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, ambapo wamejadiliana masuala kadhaa yanayohusu maendeleo ya sekta ya biashara na uwekezaji katika nchi wanachama hususan masuala ya kodi na pia wamezindua Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software) wa Kushughulikia Upatikanaji wa Taarifa za Viwango vya Ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar anayesimamia masuala ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Shariff Ali Shariff (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigae (wa kwanza kulia).

Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akizindua rasmi Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software) wa Kushughulikia Upatikanaji wa Taarifa za Viwango vya Ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCTIFI) uliofanyika tarehe 31 Mei, 2024, Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, ambapo wamejadiliana masuala kadhaa yanayohusu maendeleo ya sekta ya biashara katika nchi wanachama hususan masuala ya kodi. Wengine katika picha kulia ni Mawaziri wa Fedha, Uchumi, na Mipango wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Wajumbe mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) wakati akizindua Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software) wa Kushughulikia Upatikanaji wa Taarifa za Viwango vya Ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCTIFI) uliofanyika tarehe 31 Mei, 2024, katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, ambapo wamejadiliana masuala kadhaa yanayohusu maendeleo ya sekta ya biashara katika nchi wanachama hususan masuala ya kodi. 

Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), akichangia jambo wakati wa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCTIFI) uliofanyika tarehe 31 Mei, 2024, katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, ambapo wamejadiliana masuala kadhaa yanayohusu maendeleo ya sekta ya biashara katika nchi wanachama hususan masuala ya kodi, pia wamezindua Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software) wa Kushughulikia Upatikanaji wa Taarifa za Viwango vya Ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kulia walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wenzake wa Fedha, Uchumi, Mipango, Viwanda na Biashara kutoka nchi wanachama  wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, baada ya kutamatika kwa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCTIFI) uliofanyika tarehe 31 Mei, 2024, Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, ambapo wamejadiliana masuala kadhaa yanayohusu maendeleo ya sekta ya biashara na uwekezaji katika nchi wanachama, hususan masuala ya kodi, pia wamezindua Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software) wa Kushughulikia Upatikanaji wa Taarifa za Viwango vya Ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Katikati walioketi ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Forodha, Biashara na Masuala ya Fedha, Bi. Annette Ssemuwemba Mutaawe.

Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiagana na Waziri wa Fedha wa Uganda, Mhe. Henry Musasizi, baada ya Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCTIFI) uliofanyika tarehe 31 Mei, 2024, Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, ambapo wamejadiliana masuala kadhaa yanayohusu maendeleo ya sekta ya biashara na uwekezaji katika nchi wanachama hususan masuala ya kodi, na pia wamezindua Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software) wa Kushughulikia Upatikanaji wa Taarifa za Viwango vya Ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika wanachama wa Jumuiya hiyo.

Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar anayesimamia masuala ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Shariff Ali Shariff (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigae (wa kwanza kulia), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCTIFI) uliofanyika tarehe 31 Mei, 2024, katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, ambapo wamejadiliana masuala kadhaa yanayohusu maendeleo ya sekta ya biashara na uwekezaji katika nchi wanachama hususan masuala ya kodi, pia wamezindua Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software) wa Kushughulikia Upatikanaji wa Taarifa za Viwango vya Ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)

Na Benny Mwaipaja, Arusha

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaongoza Mawaziri wa Nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software), utakaorahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kiforodha. 

 

Uzinduzi huo umefanyika wakati wa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha.

 

Dkt. Nchemba alieleza kuwa kupitia Mfumo huo watumiaji watapata taarifa mbalimbali kuhusu viwango vya pamoja vya ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.  

 

Aidha, alisema kuwa Mfumo huo umelenga kurahisisha uchakataji na ufuatiliaji wa maombi ya unafuu wa ushuru wa forodha (duty remission) hivyo kupunguza urasimu pamoja na muda wa kupata huduma hizo.

 

Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliikumbusha Kenya, kutekeleza matakwa ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory) ya kuweka maafisa wa forodha wa Kenya nchini Tanzania watakaofanya ukaguzi wa mizigo inayotoka ama kupitia Tanzania kwenda Kenya.

 

Dkt.Nchemba alieleza kuwa Tanzania imetekeleza Matakwa ya Himaya Moja ya Forodha kwa kuweka maafisa Forodha wa Tanzania upande wa Kenya takribani miaka kumi iliyopita lakini Kenya haijafanya hivyo hatua ambayo inaiathiri Tanzania katika ufanyaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili.

 

Miongoni mwa athari hizo kwa upande wa Tanzania ni pamoja na kuwepo kwa kadhia ya ucheleweshaji wa mizigo inayotoka Tanzania kwenda Kenya kitendo kinachowaongezea wafanyabiashara gharama, kuwapotezea muda pamoja na msongamano katika mipaka ya Tanzania na Kenya ikiwemo Namanga, Holili, Horohoro na Sirari.

 

Kwa upande wake Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kenya, Mhe. Peninah Malonza alisema kuwa Nchi yake itatekeleza Matakwa ya Himaya Moja ya Forodha na kuwaweka maafisa wake wa forodha nchini Tanzania ifikapo Julai Mosi mwaka 2024, ili kundoa vikwazo hivyo vya kibiashara.

 

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Forodha, Biashara na Masuala ya Fedha, Bi. Annette Mutaawe, alisema kuwa pamoja na mambo mengine, mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa ambapo lengo kuu la kutano huo lilikuwa ni kujadili masuala ya kuimarisha biashara na uwekezaji katika nchi wanachama.

Related Posts