Kelvin John apata timu Denmark aondoka Genk

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kelvin John (20) ameondoka Club ya KRC Genk ya Ubelgiji na kwenda kujiunga na Club ya Ålborg FC iliyopanda daraja na sasa itacheza Ligi Kuu Denmark msimu wa 2024/2025.

Kelvin John inaripotiwa kuwa amesaini Mkataba wa miaka minne wa kuitumikia Aalborg FC na sasa msimu ujao tutamuona akicheza Ligi Kuu ya Denmark baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha KRC Genk licha ya awali kutangazwa kuwa alipandishwa timu ya wakubwa.

Aalborg FC ni timu kongwe nchini Denmark ilianzishwa 1885,’ ilishuka daraja msimu 2022/2023 na msimu wa 2023/2024 imepanda daraja na kurudi Ligi Kuu baada ya kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi daraja la kwanza Denmark (NordicBet League).

Related Posts