RC CHALAMILA SHULE ZINAZOJENGWA DAR ES SALAAM SASA NI GHOROFA TU

 

 

 

 Na Humphrey Shao 

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema Jiji la Ilala pamoja na Halmashauri za Manispaa ya mkoa wa Dar es salaam Ni marufuku Kuendelea Kujenga ujenzi wa Msambao  Kwa sababu ya Ardhi yake haipo kama ya mikoa mingine  

Hayo ameyasema Leo Tarehe 30 Mei 2024 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema ujenzi huu wa ghorofa ndo ujenzi unaotegemewa kuonekana Katika Jiji la dar es salaam, Wilaya na Halmashauri zingine za mkoa wa Dar es salaam 

“Ukiona majenzi mengine yakijengwa itakuwa ni ushamba mkubwa sana kwenu nyinyi watoto wangu kama mukiondoka hapa na division 4 au division 0 Kwa majengo haya,musome Kwa bidii,muwe na nidhamu,muwena heshima na Nia ya kuweza kufanya vizuri Katika mitihani yenu”. Amesema Chalamila 

Shule ya sekondari ya minazi mirefu iliyojengwa Kwa gorofa ambayo imegharimu Kwa kiasi ya shilingi Bilioni 1 na milioni 700 iliyopo Katika maeneo ya gongolamboto,Kipawa

Pia Chalamila Amesema Serikali imeandaa mikakati Kwa kila Mwalimu wa shule za sekondari kuvaa sare za kitambaa Cha suti Katika Jiji la mkoa wa Dar es salaam 

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema wameandaa baadhi ya uniform za walimu ambazo zitakazotumika Katika mikutano Mbalimbali 

Amesema baada ya kitambaa hicho itakuja na pesa ya shilingi elfu 80 cash Kwa kila Mwalimu Elfu 50 itakuwa Kwa ajili ya kiatu na elfu 30 Kwa ajili ya mashono

Related Posts