Abdulwahab Issa kutoka Roboteck Lab akitoa maelezo wakati alipotembelea banda la MUHAS
KAMPUNI ya Roboteck Lab imekutana na wabunifu kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili( MUHAS) kwa ajili ya kuwapa elimu juu ya kuwa na bunifu zinazozingatia kiwango vya kimataifa.
Akizungumza mapema wiki hii katika maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu jijini Tanga Mtaalam wa Teknolojia ya Tehama kutoka Roboteck Abdulwahab Issa, amewataka wabunifu kutoka MUHAS kushirikiana na wataalamu wa masuala ya program tumizi ( Applications) ili kuwasaidia kuwa na bunifu zenye viwango na zinazofuata taratibu za nchi.
“Kampuni yetu inatoa msaada wa kitaaluma kwa anayehitaji tupo tayari kushirikiana katika kuhakikisha bunifu zenu zinafata viwango vya kimataifa”’, amesema. Issa.
Dkt. Nelson Masota, Mratibu wa Ubunifu wa MUHAS
amesema Chuo hicho kikishirikiana na Roboteck kitaandaa mafunzo maalum ya kukuza na kuendeleza bunifu za wasomi wa chuo hicho ili kufikia viwango vya kimataifa.
“Kurugenzi ya Tafiti, machapisho na Ubunifu ya MUHAS itaisaini mkataba na Roboteck wa kuendesha mafunzo maalumu yatakayoboresha kazi za wabunifu wetu”