Mwanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Klaivet Steven akizungumza kuhusiana na ubunifu wake wa kusaidia mtu kupata makazi ya kupanga katika mikoa yote nchini.
Mwanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Paul Reuben akizungumza kuhusiana na ubunifu zao la Korosho mteja kupata korosha moja kwa moja kutoka kwa katika mfumo.
Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo katika Banda la TIA kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal Mjini Tanga.
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV Tanga
WANAFUNZI wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wamesema Taasisi hiyo wamekuwa msaada mkubwa katika kuendeleza bunifu zao kuona mbeleni kwao kutaleta matokeo chanya.
Wanafunzi hao wamesema hayo katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ubunifu yanayoendelea katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal Mjini Tanga.
Mwanafunzi wa Shahada ya Masoko na Uhusiano wa Umma Klaivet Steven amesema katika ubunifu alioufanya ni changamoto ya jamii ya kupata makazi ya kupanga na kubuni programu Nunuzi ‘APP’ ya kufanya mtu kuingia na kutafuta makazi katika mtandao sehemu yeyote kwa viwango anavyohitaji makazi (Nyumba).
Amesema programu hiyo ni DALA RESIDE HUB ambayo mtu yeyote akiingiza program hiyo kwenye mtandao anapata kila hitaji ya makazi anayotaka na kwenda kulipia.
Amesema kuwa katika Ubunifu huo kwao hawategemei kupata fedha kwa wenye nyumba au makazi wanaopangisha bali wao wanapata matangazo ndio yanakwenda kuwalipa kutokana na ubunifu walioufanya.
Amesema matokeo hayo waliopata kumetokana na Taasisi kuwa bega kwa bega nao kwanzia hatua ya kwanza hadi mwisho na kuendelea kuwafatilia kwa ukaribu.
Mwanafunzi wa Shahada ya Ugavi na Usafirishaji Paul Reuben amesema katika Ubunifu wao wamejikita katika zao la korosho ambapo wanunuzi wa korosho wakitaka wanaingia katika program Nunuzi ‘APP’ ya CashewnutTz.Online na kwenda kununua hizo hizo korosho wanazohitaji katika mfumo.
Amesema kuwa wenye zao korosho wanaingiza taarifa zao katika mfumo na aina ya korosho na wanalipia katika kuingiza taarifa hizo.
Amesema kuwa zao la korosho lina maeneo matatu ambapo mteja anayetaka kununua anapata kile anachohitaji kwenye zao la Korosho.
Reuben amesema kuwa suala la kujiajiri ni fursa kwao kutokana na kuanza kwao mapema hata anavyohitimu anajua cha kufanya.