Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kushirikiana na Serikali ya Norway katika sekta mbalimbali.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes aliyefika Ikulu Zanzibar kwa kujitambulisha tarehe:30 Mei 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi alimueleza Balozi Tinnes kuwa Zanzibar imeendelea kunuifaika na fursa nyingi kutoka Norway na ipo tayari kuendeleza ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati ya umeme kuwajengea uwezo watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).
Pia Sekta ya mazingira, utalii, afya, elimu, Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Mafuta na Gesi.
Naye, Balozi Tinnes amesema Norway itaendelea kudumisha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia uliopo na kuendeleza ushirikiano kwenye sekta mbalimbali .