Na Mwandishi wetu, Michuzi Tv
GS1 Tanzania wazindua Barcodes Charity Wark kwa lengo la Kusaidia wanawake 100 kutoka kila Wilaya hadi kufikia Wanawake 18300 ili kupata alama ya msimbomilia (Barcodes) katika bidhaa wanazozizalisha.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo, Juni Mosi, 2024, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Sempeho Manongi amesema Serikali imejikita katika kutafuta Masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini pia imejikita katika kufungua fursa za kibisahara kwa maana ya kufungua na kuboresha mazingira yasiyorafiki kwenye biashara ili kuvutia wanawakewengi zaidi kufanyabishara.
“Kwahiyo nchi yetu imefunguka kwa ukubwa mara baaada ya kusaini mikataba ya kibiashara, tunalo soko huru la Afrika, soko la Afrika Mashariki, soko la nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara (SADEC), pia tunaweza kupeleka bidhaa kwenye soko la bara la Ulaya, Asia, Amerika kupitia programu ya AGOA na tunanafasi kubwa ya kupeleka bidhaa zetu tunanzozizalisha.
Manonga amesema ili Wananwake waweze kupeleka bidhaa katika masoko hayo, lazima iwe na historia, lakini kwa kutumia Barcodes ni njia rahisi zaidi kuhifadhi historia hiyo.
Amesema Barcodes hiyo ndio utambulisho wa bidhaa kwenye ulimwengu Wa Kidijitali ambapo alama hiyo Ukiiscan inaonesha kwamba nani ameizalisha, ni bidhaa gani na inamtambulisha mfanyabishara kwa mteja kwa kutumia njia rahisi na kahuna namna inawezekana kuikwepa biashara hiyo.
Manongi amewaasa Wanawake kuwa lazima wawe na Barcode Msimbomilia kwenye bidhaa zao ili uweze kutambulisha bidhaa sokoni kwani utambulisho huo ni wa kipekee kwaajili ya kubadilisha mwenendo wa mfanyabishara lakini pia kuongeza wigo mkubwa wa kipato kwenye bidhaa tunazozizalisha.
“Saa imefika ya kuipeleka barcode vijijini ili iweze kufaidi masoko ya nje ya nchi na huwezi kufanya hivyo bila ya kuwa na msimbomilia(Barcode) huwezi kupata taarifa za wapi bidhaa imezalishwa bila ya kuwa na barcode.
Kwahiyo akinamama muda umefika sasa kushirikiana na Serikali, Wizara ya Viwanda na Bishara, TIRDO, na GS1 kupitia Program ya Charity Work kwaajili ya Kufanikisha akinamama 100 wa Kila halmashauri za Wilaya zote nchini akinamama kujiunga na barcode.
Manongi ameeleza kuwa anatakiwa kuongeza mauzo sokoni, tunaongeza fedha za kigeni, fedha za kigeni zikiingia nchini tunajenga uwezo mkubwa wa uzalishaji, tunaongeza ajira, pato linaongezeka familia zinaboreka uchumi wa kaya unaongezeka na maisha yanakuwa bora hilo ndio lengo la Serikali.
Pia amesema kuwa Wanawake wanajukumu la kutambulisha bidhaa kwenye masoko ya kidijitali ili ziweze kufahamika kokote duniani lakini ni lazima kuzingatia ubora na usalama na vigezo vyote ili viweze kufanikisha upatikanaji mazuri na ya kudumu ili kuweza kupata mapato zaidi.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa GS1Tanzania, Fatma Kange amesema kuwa msimbomilia unaonesha kuwa bidhaa hii imetoka Tanzania hasa ikianza na namba 620…. Na ukiona Msimbomilia unaoanzaia na namba 698…. haielezei kama bidhaa hiyo inatoka Tanzania.
Amesema kuwa Matembezi hayo yatasaidia Wanawake kutangaza bidhaa zao kwenye masoko ya Kimataifa kidijitali zaidi. Dijitali sio kutumia mitandao ya kijamii tuu bali na hata kwenye bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini.
Fatma amesema kuwa lazima kupeleka bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kwenye masoko hayo.
“Hii barcodes ili iweze kuwafikia wanawake GS1 wamepunguza bei kutoka shilingi 235000 hadi kufikia sh. 75000. Sasa lazima zifike kwenye migebuka kwasababu gharama zimeshuka ili wanawake waweze kuwafikia masoko ya kimaifa.”
Baadhi ya wanawake waliohuduria uzinduzi wa Uzinduzi GS1 Tanzania Barcodes Charty Walk ambayo imeanza leo June Mosi na kuhtimishwa Septemba 15, 2024.