Husna Sekiboko atekeleza Maelekezo ya Mwenyekiti wa UWT Taifa

Raisa Said,Tanga

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Husna Sekiboko leo tarehe 29 May 2024 ametekeleza agizo la Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mama Mary Chatanda la kuchangia Simu kwaajili ya usajili wa wanachama wa CCM na UWT.

Katika utekelezaji huo Sekiboko amekabidhi simu 10 zenye thamani ya sh. Million 4, kwa Makatibu na Wenyeviti wa Jumuiya hiyo kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Tanga.

Hata hivyo Wenyeviti na Makatibu hao kutoka Wilaya za Tanga, Lushoto, Mkinga, Pangani, Handeni, Korogwe, Muheza, Kilindi, vijijini na Mjini walimshukuru Mbunge Sekiboko nakusema ameleta simu hizo wakati muafaka chama kikiwa na mkakati wa kusajili wanachama wengi ikiwa ni moja ya nyenzo ya ushindi wa Kishindo kwa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.

Kwa upande wake Sekiboko amesema anafurahi kutekeleza agizo hilo ikiwa ni moja ya mchango wake wa kuhakikisha RAIS SAMIA SULUHU HASSAN anapata ushindi Mkubwa wa kihistoria katika uchaguzi kuu wa mwaka 2025.



Related Posts