MAELFU YA WANANCHI WAFURIKA KUAGA MWILI WA BABA MZAZI WA MBUNGE KOKA

NA VICTOR MASANGU,KILIMANJARO

Maelfu ya  wananchi,viongozi, wa serikali,wakiwemo mawaziri  wakuu wa Wilaya wakuu wa Mikoa,Wabunge  viongozi wa  dini,madiwani na viongozi wa mashirika wamejitokeza kwa kwa ajili ya kumzika aliyekuwa Baba mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini mzee Francis Koka  katika nyumba yake ya milele.

Mazishi hayo ambayo yamefanyika nyumbani kwa marehemu  katika eneo la kijiji cha Mkolowonyi kata ya Mvienyi  mkoani Kilimanjaro  yameweza pia kuhudhuriwa  na mwakilishi wa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan Felister Mdeme  pamoja na wawakilishi wa wabunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akitoa salamu za rambi rambi  kwa niaba ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  mwakilishi  wake Felister Mdeme ametoa pole kwa familia ya Mbunge Koka  kutokana na kufiwa na baba yake.

“Nimeagizwa na Rais Samia kuja hapa Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuweza kutoa pole kwa familia ya Mh.Mbunge Koka na amesema kwamba yupo pamoja nanyi  katika msiba huu,”alisema Mdeme kwa niaba ya Rais Samia.

Mwakilishi huyo  wa Rais alibainisha kwamba Rais Samia angependa kufika katika shughuli hiyo ya mazishi mkoani Kilimanjaro lakini ameshindwa kufika kutokana na ratiba kuingiliana lakini atayaenzi yote ambayo yameachwa na marehemu mzee Francis.

Akitoa salama za rambi rambi kwa niaba ya Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ramadhani Mlao amempa pole Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuondokewa na baba yake mzazi.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake wa Mkoa wa  Pwani Muharami Mkenge alibainisha kwamba wabunge wote wametoa  salamu za pole kwa  Mbunge Koka kwa kuondokewa na baba yake na kwamba wapo pamoja naye katika kipindi hiki kigumu.

Katika msiba huo pia Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka alitoa pole kwa familia ya Mhe.Mbunge na kuwahimiza kuwa wavumilivu hasa katika kipindi hiki cha majonzi.

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Taifa  (CHADEMA) Freeman Mbowe alikuwepo katika msiba huo alisema kwamba wameguswa na msiba wa baba yake mzazi na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini na kwamba wapo pamoja katika kipindi hiki cha mahombolezo.

Kwa upande  wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ameshukuru viongozi mbali mbali wa vyama na serikali pamoja na wananchi kwa namna jinsi walivyojitoa kushiriki katika mazishi ya baba yake.

“Kwa kweli marehemu baba yangu amefariki akiwa na umri wa miaka 104 na alishawahi kupigana vita vya pili vya dunia,kwa hivyo kitu kikubwa inabidi tuyaenzi yale yote na ninawashukuru kwa dhati viongozi na wananchi wote kwa ujumla wake ambao wamefia katia msiba huu, “alifafanua Mhe.Koka.

Pia katika msiba huyo ulihudhuliwa na Wakuu wa mikoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo ambao wametoa salamu zao za pole kwa familia ya Mbunge Koka.

Waziri wa ardhi Jerry Slaa naye alikuwa ni mmoja wa wahombolezaji alitoa salama za pole kwa niaba ya mawaziri wenzake ambao wengine walishimdwa kufika kutoka na bunge la bajeti.

Nao viongozi wa  wa dini ambao walioendesha Ibada ya misa  takatifu  aliwasisitizia wahombolezaji kuhakikisha kwamba kuwa na upendo wakati wa maisha yao na kijifunza na kwamba wayaishi yale yote mazuri ambayo ameyaacha wakati wa uhai wake.

Vingizi huyo hawakusita kumwelezea Mbunge Koka pamoja na marehemu baba yake kwa jinsi walivyokuwa mstari wa mbele katika kushirikiana bega kwa bega na wananchi katika mambo ya maendeleo.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mkolowonyi walisema kwamba familia ya Mbunge Koka imekuwa karibu na jamiii katika kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Marehemu mzee Francis Koka alizaliwa Juni 6/1920 alifariki dunia mnamo Mei 22 mwaka huu wa  2024 akiwa na umri wa miaka 104 na amezikwa leo nyumbani kwake katika kijiji cha Mkolowonyi Kata ya Mvienyi mkoani Kilimanjaro.


Related Posts