Mwakinyo mambo magumu, msimamizi WBO atoa masharti haya

Hali bado si shwari kwa bondia Hassan Mwakinyo, kutokana na tukio la kushindwa kupanda ulingoni jana usiku kuzipiga na  Mghana, Patrick Allotey kutetea ubingwa wa WBO Afrika.

Mwanaspoti linalofuatilia kikao cha kujadili mipangto ya pambano hilo kurudiwa baada ya kukwama jana jiji Dar es Salaam kilikuwa hakijatoa muafaka hadi muda huu, kwani bado kuna mvutano ya juu ya kufanyika tena kwa pambano hilo, huku Msimamizi wa mkanda wa WBO Afrika katika uzani wa middle, amewapa masharti waandaaji wa wasimamizi wa pambano hilo kuwa, hadi kufikia saa 12 awe ameshalipwa pesa zake ili aruhusu wawili hao kuzichapa.

Inadaiwa Msimamizi huyo, Samir Captain kutoka Ghana, amechimba mkwara kwamba, ikishapita muda huo yeye atakuwa akijiandaa na safari ya kurudi kwao usiku wa leo na Mwakinyo atakuwa amevuliwa ubingwa wa WBO Afrika

Hata hivyo, bado baadhi ya maofisa wa WBO wa hapa nchini wamedai kuna juhudi za watu kusaka ukumbi mpya Masaki kwa ajili ya pambano hilo lipigwe leo licha ya kuwa bado Mwakilishi na Msimamizi hajawekewa pesa yao ili kuruhusu Mwakinyo na Allotey kuzipiga upya.

Related Posts