NA VICTOR MASANGU, PWANI
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani ndugu David Mramba katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya michezo anatarajia kuanzisha mashindano maalumu ya mbio za miguu zitakazojulikana kwa jina la Samia One Marathon ambazo zitazishirikisha taasisi mbalimbali zinazofanya shughuli zake ndani ya Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake kuhusiana na maandalizi hayo Mwenezi alisema kwamba lengo kubwa la kuanzisha mashindano hayo ni kwa ajili ya kuweza kukuza mchezo huo wa riadha, kubadilishana mawazo na wadau mbali mbali wa Mkoa wa Pwani ili kuweza kuimarisha mahusiano baina ya chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na wadau na taasisi ikiwa sambamba na kujenga afya zao.
Mramba alisema kwamba katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika Juni mwaka 2024 yataweza kuwakutanisha wadau mbali mbali wa michezo zikiwemo taasisi za kiserikali pamoja na taasisi nyigine ambazo sio za kiserikali pamoja na vyamba vingine vya michezo ili kuweza kukutana kwa pamoja na kufanya mambo mbali mbali ikiwemo kukimbia na kubadilishana mawazo.
“Kwanza kabisa nipende kutoka shukrani zangu za kipekee kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali katika Mkoa wa Pwani kwani waliweza kunishika mkono na kunipasapoti kubwa hivi karibuni pindi nilipoandaa kikao changu maalumu ambacho kiliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwamba ninawaomba tushirikiane kwa pamoja siku ya tukio kubwa la mbio hizo ambalo litakuwa la kihistoria,”alisema Mramba.
Kadhalika Mramba alifafanua kwamba ana imani kwamba kupitia mashindano hayo ya mbio hizo za Samia One Marathon zitaweza kuleta matokeo chanya kwani zitatoa fursa ya wadau mbali mbali pamoja na taasisi hizo kuonyeha uwezo na vipaji vyao walivyonavyo katika sekta ya mchezo huo wa Riadha.
Mwenezi Mramba alibainisha kwamba katika michuano hiyo taasisi hizo na wadau watapa fursa ya kuweza kukimbia mbio za kuanzia kilometa zipatazo tano,kumi,hadi kilometa 21 ambapo washindi wote watazawadiwa zawadi mbali mbali kwa ajili ya kutambua mchango wao katika kufanya vizuri.
Katika hatua nyingine Mwenezi huyo alisema kwamba fomu kwa ajili ya ushiriki wa mashindano hayo zitaanza kutolewa mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu na kwamba zitapatikana katika ofisi za mwenezi wa CCM Mkoa wa Pwani na kuwahimiza washiriki wote wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu hizo.
Katika hatua nyingine Mwenezi huyo alitoa wito kwa wadau michezo, wananchi,taasisi mbali mbali za Mkoa wa Pwani kumpa sapoti ya kutosha kwa lengo la kuweza kufanikisha michuano hiyo ya Samia One Marathon ambayo ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa vitendo katika kukuza sekta ya michezo hususan mchezo wa Riadha.