SERIKALI YAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WACHIMBAJI WADOGO – CHUNYA

 


SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wadogo kuhakikisha wanapata mitaji, leseni  na matumizi ya teknolojia katika shughuli za uchimbaji wa madini

Hayo yamesemwa na Afisa Madini Mkazi Chunya, Mhandisi Laurent Mayala wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatembelea wachimbaji wadogo katika eneo la Itumbi.

Amesema, Serikali inaendelea kuhamasisha mabenki kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wachimbaji wadogo ili kuweza kutatua changamoto ya mitaji yao.

“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wadogo kwa kutoa vifaa vya kisasa ambapo imesaidia sasa hivi kuchimba madini kwa uhakika,”amesema Mayala.

Pia, amefafanua kuwa jitihada hizo zimechangia kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli ya Serikali hadi kufikia shilingi bilioni 33 kutoka shilingi bilioni 30.4 ikiwa ni lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Kwa upade wake mchimbaji mdogo wa kampuni ya Achimwene Bussiness Group Company Limited, Heneriko Maganga amepongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuweka mazingira wezeshi ikiwemo bei nzuri sokoni ili wachimbaji wadogo waweze kunufaika zaidi.

Amesema wataendelea kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa ajira kwa vijana na kurudisha faida kwa kile kinachopatikana katika vijiji vinavyozunguka migodi.

“Serikali imerahisisha vitu vingi ikiwemo kuhakikisha bei ya dhahabu sokoni zinakuwa juu ili wachimbaji wadogo wanufaike. Tumeendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kurudisha faida kwa jamii ikiwemo kununua kompyuta katika Shule ya Sekondari ya Matundasi, kutoa misaada kwa wasiojiweza  na kushiriki katika ujenzi wa Sekondari ya Masache,”amesema Mayala.

Naye mchimbaji mdogo Hamad Shaban ameiomba Serikali kutilia mkazo suala la wachimbaji wadogo kutumia leseni zao kama dhamana ya kupata mikopo ili kukabiliana na chagamoto ya mitaji.

Related Posts