TARI yaja na Utafiti wa Mbolea zinazotokana na taka

Mtafiti wa Udongo na Mbolea wa Kituo cha Serian Arusha Richard Temba akionesha Utafiti wa Mbolea unaotokana na taka ambazo baada ya uhifadhi zinazalisha minyoo ya kufanya uchakataji wa Mbolea ambapo Elimu ya Utafiti na Ubunifu ulitolewa katika Maadhimisho ya Elimu, Ubunifu na Ujuzi yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal Mjini Tanga.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Tanga
TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ubunifu na Ujuzi wameonyesha Utafiti walioufanya wa Mbolea ambao unaweza kufanyika kutokana na taka mbalimbali.

Mtafiti wa Udongo na Mbolea Kituo cha Utafiti TARI Serian Arusha Richard Temba amesema kuwa Takataka zinazozalishwa majumbani zinaweza kutengeneza Mbolea na kuweza kutumika katika Kilimo.

Temba amesema hakuna sababu wa Taka zinazozalishwa majumbani ukalipia wakati zinaweza kuleta uchumi kutokana taka hizo.

Amesema taka zilizo masokoni zikihifadhiwa baada ya muda zinatengeneza Mbolea na kutumika katika Kilimo.

Temba amebainisha kuwa taka ambazo zinazalishwa zinaweza fedha kwani zinaweza kununuliwa na kwenda kutumi kwa ajili ya mbolea.

Amesema Mbolea za taka zikitumika katika mashamba haziharibu Udongo ambapo hata mazao baada ya kutoka mabaki take tena yanawekwa kwa ajili ya mbolea.

Related Posts