WAHADHIRI NELSON MANDELA WATUNIKIWA VYETI KWA KUCHAPISHA TAFITI ZA KIMATAIFA

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa (kushoto) mara baada ya kumkabidhi cheti Mhadhiri kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Emmanuel Mpolya (kulia) ambaye ni miongoni mwa Wahadhiri waliopata tuzo kwa kuchapisha tafiti katika majarida yenye hadhi ya kimataifa.

……..

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewapongeza na kuwatunuku Vyeti Wahadhiri wanne kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela baada ya kushinda tuzo ya kuchapisha matoleo ya kiutafiti katika majarida yenye hadhi ya kimataifa.

Wahadhiri waliotunukiwa vyeti ni Prof. Karoli Njau, Prof. Joram Buza, Prof Anael Nkya na Prof. Emanuel Mpolya ambao waliotunukiwa wakati wa kilele cha kufunga maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa Elimu, Ujuzi na Ubunifu Mei 31,2024, jijini Tanga.

“Naipongeza taasisi ya Nelson Mandela kwa kutoa elimu iliyojikita katika kutatua changamoto za jamii kupitia tafiti na bunifu mbalimbali zinasosaidia katika kuinua uchumi wa viwanda amesema “ Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi Prof. Lughano Kusiluka amepongeza kazi kubwa inayofanywa na taasisi hiyo kwa kuwasimamia vyema wanataaluma wenye mchango katika kuleta maendeleo ya kijamii huku akiitaka Idara ya Utafiti na Ubunifu kuendelea kusimamia wabunifu kuhakikisha bunifu hizo zinaingia sokoni.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula ametoa wito kwa wabunifu katika Taasisi hiyo kuhakikisha bunifu zote zinazoenda kwenye maonesho zinaingia sokoni ili baada ya maonesho jamii iweze kunufufaika nazo .

Maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ni muunganiko wa maonesho ya kitaifa matatu ambayo ni ni ubunifu (MAKISATU), maonyesho ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na maonyesho ya elimu ya juu Sayansi na Teknolojia TCU amabayo yalifunguliwa Mei 25,2024 na kuhitimishwa Mei 31,2024 viwanja vya Shule ya sekondali Popatlal Tanga kwa kushiriki Taasisi zote za elimu nchini.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akiongea wakati wa kufunga maadhimisho ya wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal Tanga.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa (kushoto) mara baada ya kumkabidhi cheti Mhadhiri kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Emmanuel Mpolya (kulia) ambaye ni miongoni mwa Wahadhiri waliopata tuzo kwa kuchapisha tafiti katika majarida yenye hadhi ya kimataifa.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa (kushoto) mara baada ya kumkabidhi cheti Mhadhiri kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Karoli Njau (kulia) ambaye ni miongoni mwa Wahadhiri waliopata tuzo kwa kuchapisha tafiti katika majarida yenye hadhi ya kimataifa viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal Tanga.

Makamu Mkuu waTaasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wahadhiri waliotunukiwa vyeti na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa kupata tuzo ya kuchapisha tafiti katika majarida yenye hadhi ya kimataifa wakati wa kuhitimishwa kwa maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal Tanga Mei 31 ,2024.

Makamu Mkuu waTaasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya NelsonMandela Prof. Maulilio Kipanyula (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunifu wa Taasisi hiyo walioshiriki katika Wiki ya Kitaifa Maadhimisho ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yaliyohitimishwa Mei 31, 2024 viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal Tanga Mei 31 ,2024.

Related Posts