WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza halmashauri zote nchini, kuhakikisha kwenye maeneo yao zinaanzisha madawati ya sayansi,teknolojia na ubunifu, ili kuweza kukuza na kulea bunifu mbalimbali katika halmushauri kwa vijana waliopo kwenye sehemu hizo.
Hayo aliyasema.wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kitaifa ya elimu,ujuzi na ubunifu 2024 ,yaliofanyika mkoani Tanga.
Alisema kwa kufanya hivyo itaweza kusaidia vijana kuweza kujiendeleza na kuhifadhi bunifu hizo kwaajili ya kuweza kutumika kwenye maeneo na mamlaka husika.
Waziri mkuu ameiagiza wizara ya elimu na taasisi za umma na binafsi kuhakikisha sera ya elimu ya 2024,inatekelezwa vizuri na kufanyiwakazi kama ilivyokusudiwa,kwani bila kufanya hivyo haiwezi kuleta manufaa yoyote yale kwa jamiii.
Alisema Serikali imekamilisha mapitio ya sera ya elimu 2024,ambapo utekelezaji wake umeanza Januari mwaka huu,ambayo inamhisisha kijana kuweza kujifunza mambo mbali ya kuweza kujiajiri.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kwa upande wake alisema kwasababu ya uhaba wa wataalam wa masuala ya Nyuklia serikali imeweka mpango wa kuwasaidia vijana kwenda nje kusomea mambo hayo,lengo likiwa ni kuongeza wataalam hao nchini.
Alisisitiza serikali inaendelea kuwabeba wabunifu waliogundua na kubuni vifaa mbalimbali,kuwatafutia soko kwaajili ya bunifu hizo mbalimbali ambazo wamegundua ili na wao waweze kujipatia kipato.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge wa Kamati ya elimu,
utamaduni na nichezo Husna Sekiboko alieleza serikali iangalie jinsi ya kuzitumia bunifu zilizoonyeshwa,kwani zinatakiwa kutumika na kuleta faida kwenye jamii na sio katika maonyesho pekee.
Alisema kila taasi ambayo kuna bunifu inawagusa waichukue na kuangalia utaratibu wa kuweza kuangalia wanaweza kuitumia vipi na kuleta faida kwenye jamii na bunifu husika kuwa na tija.
Mshiriki wa maadhimisho hayo Msajili msaidizi wa Chuo Kikuu cha The Aga Khan Agath Damas aliipongeza serikali kwa maadhimisho hayo,ila kushauri pia nguvu iwekwe kuhamasisha,wanafunzi kupenda masomo ya sayansi,kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza idadi ya wataalam hao nchini.
Alisema watoto wengi wamekuwa na uoga sana wa masomo ya sayansi,hivyo upo umuhimu wa kuwashauri kuwa masomo hayo nayo yana umuhimu wake,katika jamiii,na lazima wataalam wa sayansi wapayokane nchini.
Maadhimisho ya kitaifa ya elimu,ujuzi na ubunifu 2024 yalikuwa na kauli mbiu inayosema elimu,ujuzi na ubunifu kwa uchumi shindani.