BALOZI NCHIMBI AZINDUA SHINA LA WAKEREKETWA WAJASIRIAMALI TARIME GROUP


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akizindua Shina la Wakereketwa Wajasiriamali, Tarime Group lenye wanachama 200, ambalo lipo eneo la Makuyuni, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha

Dkt Nchimbi amewasili Arusha, tayari kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake kwenye mikoa mitano, ya Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, akiwa amembatana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Hamid Abdallah.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mataves, katika eneo la Kitongoji cha Kisongo, Kijiji cha Ngorbob, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, na kusikiliza kero zao na kuzitafutia majawabu, ambapo pia alizindua Shina la Wakereketwa wa CCM Akinamama Wajasiriamali wa Soko la Kisongo, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo, leo Jumapili Juni 2, 2024.




Related Posts